Waziri Mkuu Wa Madagascar Ajiuzulu.

Olivier Mahafaly Solonandrasana Waziri Mkuu wa Madagascar ametangaza kujiuzulu katika kipindi ambacho nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na mgogoro wa kisiasa, ambapo kuanzia sasa serikali ya umoja wa kitaifa inatarajiwa kuundwa.
Olivier Mahafaly Solonandrasana amechukua hatua hiyo ni kufuatia ombi la mahakama kuu ya katiba katika hali ya kumpata waziri mkuu mpya kutoka makubaliano baina ya wanasiasa.
Hivi karibuni Mahakama Kuu ya Katiba ilitoa agizo kwa rais wa Madagascar kufuta serikali yake na kumteua waziri mkuu mpya anayeungwa mkono na vyama vyote vya kisiasa nchini humo.
Hii ni hatua ya kwanza kueekea uteuzi wa waziri mkuu mpya kutoka makubaliano katika hali ya kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Madagascar.

Mnamo mwezi Aprili Madagascar ilikumbwa na maandamano yaliyosababisha maafa makubwa dhidi ya sheria mpya za uchaguzi ambazo zingeliweza kuzuia aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marc Ravalomanana kuwania katika uchaguzi wa urais, kwa mujibu wa wafuasi wake.

Comments