Afisa Tawala Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, Ally Mketo amewahiza
walimu wa shule mbalimbali za msingi Wilayani hapa wanaowasimamia wanafunzi
wamichezo ya umitashumita wahakikishe wanashika namba moja kimukoa.
Mketo aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa michezo ya
wanafunzi umitashumita katika viwanja vya shule ya Sekondari Ushirombo wanafunzi hao wanafanya michezo kwa siku tano
kisha wanaenda kukutana na timu zingine za michenzo mbali mbali.
Alisema walimu wa michezo wahakikishe ushindi kimukoa
wanauleta Bukombe kwa kuzingatia misingi ya michezo na miongozo mizuri kwa wanamichezo kwa
kuzingatia nidham na upendo baina yao.
Kwa upande wake Afisa michezo
Wilaya ya Bukombe Jenipha Kisusi alisema kuwa michezo hiyo ya
umitashumita umeshirikisha wanafunzi toka tarafa ya Siloka, Ushirombo, Bukombe
na wanafunzi wanao shiriki 209 wavulana
126 wasichana 83 walimu wa michezo 21 wakiume 14 wakike 7.
Kisusi alisema wanafunzi hao wanashiriki michenzo ya mpira wa
miguu, Pete, wavu, mikono,sanaa na riadhaza aliongeza kuwa ndani ya mafanikio
hayo ya kuwapata wanafunzi wenye vipaji
wamekutana na changamoto za wazazi kutokuwa tayali kuluhusiu watoto wao
kushiriki na wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti
aliomba wadau wa michezo kuwachangia watoto hao ili wakafanye vizuri .
Kwa niaba ya Afisa Elimu Wilaya Sida Shalali alimuhakikishia
mgeni rasimi Afisa tawala Wilaya Ally Mketo kuwa wanafunzi na walimu wamepewa
maelekezo ya kuleta Umbingwa Bukombe aliwaomba wananchi wa wilaya ya Bukombe
kuendelea kuwaombea watoto mungu
awasaidie wafanye vizuri walete ubigwa wa michezo ya umitashumita.
Comments
Post a Comment