Viongozi wa madhehebu ya Dini Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, amewahimiza kufundisha waumini wao kuondokana na imani potofu za
kuamini ushirikina na watu wenye ualbino kuwa ni dili badala yake washirikianae
kupinga mauaji ya wazee kwa imani potofu na watu wenye ualbino kwa madai kuwa
viungo vyao ni utajili.
Wito huo ulitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eng Hamad
Masauni ambae alikuwa Mgeni rasmi katika
hafla ya kufuturisha waumini na viongozi wa dini ya waislamu Wilayani hapa iliyo
hudhuliwa na viongozi wa vyama vya siasa na serikali kutoka sehemu mbalimbali
nchini iliyokuwa imeandaliwa na Naibu Waziri wa Madini pia Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.
Masauni aliwaomba waumini wa dini ya kiislamu na mazehebu
mengine kuendeleza upendo kwa watu wote na waumini wa kiisilamu aliwasisitiza kudumu
katika imani ya kiisilamu wakati wote na kusimamia mafundisho waliyoyapata
wakati wa mwenzi mtukufu wa ramadhani.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa BAKWATA Shekh Hasan Kabeke
alisema waisilamu wengi wamekuwa wakishika imani za dini wakati wa mfungo wa
mwenzi mtukufu kisha kusahau kwa muda mfupi hali ambayo inamchukiza mwenyezi
mungu.
Kabeke aliwataka waisilamu kuwa mfano bora katika jamii kwa
kueshimu misingi ya kidini na sheria za nchi na kujikumbusha kunyeyekea na
kudumu katika mafunzo ya kiisilamu.
Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe
Mhe. Doto Mashaka Biteko aliwashukuru waislam kwa dua zao njema za kuiombea Wilaya ya Bukombe
na Tanzania kwa ujumla ili iendelee kuwa kisiwa cha amani.
Biteko aliwahimiza waislamu na waumini wa madhehebu mengine kuendelea na ushirikiano wa kuwaombea viongozi
wa serikali ya awamu ya tano ili kila wanacho kifanya kiwe na kibali cha kimungu
kwa masilahi ya taifa.
Biteko aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuhamasisha
waumini kusomesha watoto na kufanya kazi za maendeleo kwa kuzingatia sheria na
kuacha kuingiza siasa kwenye maendeleo badalayake waibuwe frusa za kiuchumi kwa
kufanya ujasilimali hali ambayo itawafanya kuongeza pato la famiiia na taifa.
Comments
Post a Comment