Watalamu wa idara ya afya,fedha,mipango na ICT kutoka katika halmashauri za Mkoa wa Geita wamepokea mafunzo ya mfumo mpya wa ugatizi wa madaraka kwa kupeleka fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za afya,mfuko wa Bima ya afya iliyoboreshwa kwa jamii ICHF pamoja na matumizi ya fedha na ununuzi wa dawa na
vifaa tiba (JAZIA).
Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu Wilayani Bukombe Katibu Tawala
wa Mkoa wa Geita Selestini Gesimba alisema mafunzo hayo yatawaimarisha ili wafanye kazi kwa ufanisi na wepesi zaidi
Gesimba alisema awali
kulikuwa na changamoto kwa wananchama wa CHF walikuwa
hawatibiwi nje ya Wilaya kabla ya kuboreshwa lakini kwa sasa kunamabadiliko makubwa yaliyofanywa
na serikali mwanachama anatibiwa Wilaya yeyote hapa nchini na kuwaomba
wanaoshiriki mafunzo hayo kuhakikisha wanawaelimisha wananchi ili wanufaike na
huduma za afya zilizo boreshwa (ICHF).
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk Japhet Simeo amekili kuwepo
kwa baadhi ya changamoto ya ucheleweshwaji wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
kwa wakati na kwamba kupitia mfumo huu mpya kutarahisisha upatikanaji wa dawa kwa
muda sahihi.
Kwa upande wake Mshauri wa Menejimenti ya dawa katika mradi huo Fiona
Chilunda alisema Serikali Mkoani Geita kupitia mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS)
ulioanza kwa kutekelezwa kwenye mikoa mitatu na hatimae nchi nzima kwa kushirikiana na
serikali ya Tanzania na Uswis imekusudia kuendelea kupunguza
changamoto za upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba kuanzia kwenye
vituo vya afya, zahanati na hospitali zote nchini.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dk Irine Mkerebe alipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa na
ushirikianao na serikali ya Uswis hali ambayo italeta mabadiliko makubwa
kutokana na mafunzo wanayopewa huku hoja hiyo ikiungwa mkono na Mganga Mkuu
wa Wilaya ya Chato Dk Athanas Ngambakubi akisema kupitia mafunzo
hayo kutasaidia kupunguza baadhi ya changamoto kwenye idara ya afya Mkoani hapa.
Comments
Post a Comment