Wanafunzi Kinshasa Waandamana Kupinga Ongezeko La Nauli.


Polisi jijini Kinshasa imesambaratisha maandamano ya wanafunzi walioandamana kupinga kupanda kwa bei ya nauli ya usafiri wa bus.
Taarifa kutoka jijini humo zimearifu kuwa wa 14 wametiwea nguvuni huku wengine 15 wakijeruhiwa wakati wa purukushani za polisi na waandamanaji.
Cedric Mbunza ambaye ni mwanafunzi ameeleza kuwa wanayo haki ya kuandamana kuitaka serikali itafute suluhu kwa tatizo hilo.
Upande wake waziri wa Elimu ya juu nchini DR Congo Steve Mbikai amesema wanafanya mazungumzo na wadau mbalimbali kutafuta suluhu kwa tatizo hilo, huku akiwataka baadhi ya wanafunzi kutohatarisha hali ya mambo

Comments