Walimu wa shule ya msingi Kata ya Namonge Wilaya ya
Bukombe Mkoani Geita, wameiomba serikali iwakumbuke walimu kuwapandisha
madaraja walimu ambao wanasifa hiyo ikiwa ni haki yao kama watumishi.
Rai hiyo ilitolewa na mkuu wa shule ya msingi Namonge Jemes Kadogo
wakati wa sherehe ya kwanza tangu 2002 shule hiyo
kuazishwa, akisoma risara kwa mgeni rasmi huku akibainisha changamoto zinazawakabili
walimu ikiwa ni pamoja na upugufu wa miundo mbinu ya shule na walimu 21 wakiwa na sifa za kupandishwa
madaraja mbali mbali ya kitaluma lakini wamekuwa wakipigwa dana dana wanapo fuatilia suala hilo.
Kadogo alimuomba Diwani wa Kata ya Namonge Mulalu Bundara ambae alikuwa ngeni rasmi kwenye
sherehe za Mei Mosi iliyokuwa imeadaliwa na walimu wa shule hiyo alisema.
“muwakilishi wa wananchi na watumishi wa umma kata ya Namonge katika vikao vya baraza la
madiwani halmashauri ya Bukombe tunaomba sana utusaidie ili ofisi ya Elimu
iwape sitahiki zao za kimsingi walimu ikiwa shule iliazishwa 2002 mpaka sasa kuna walimu 25 wanafunzi 2859 wanasitahili kusomea kwenye
vyumba vya madarasa 63 lakini wanasomea madaradasa 11 walimu wanaohitajika 62 waliopo 25 kati yao 21
wanamda mrefu hawajapandishwa madaraja”alisema Kadogo.
Muwakilishi wa CWT tawi la Namonge shule ya msingi Justina
Malifedha aliwaomba walimu wezake kuwa na ushirikiano na kufanyakazi kwa
kuzingatia mipaka ya kufanyakazi kwa kujituma ili kuinua Elimu Wilaya ya Bukombe
na Taifa kwa ujumla.
Diwani wa Kata ya Namonge Mulalu Bundara aliwaomba walimu kuwa maswala ya
kupandishwa madaraja yanataratibu zake na kuwahakikishia kuwa atalifatilia kama mwakilishi wao na aliwakumbusha
kuwa kazi ya uwalimu ni wito wahakikishe
wanaendelea kufanyakazi vizuri ikiwa shule hiyo imeingia kwenye 10 kati
ya shule 78 za Wilaya kwa mika mitatu tangu mwaka 2015.
Bundara aliwaomba walimu kutambua fursa za kiuchumi
na kuwekeza kwenye ujasiliamali wakati wakiwa na ajira serikalini ili watakapo
fikia umri wa kustaafu wasianze kujifunza kazi za ujasiliamali badala yake waanze
mapema kuzitambua fursa.
Bundara alikemea bazi ya walimu wamekuwa na tabia ya ulevi wa
kupindukia kila unapofika mwisho wamwezi wanasahau na famila zao wakidai kuwa
chezea mshahara usicheze kazi huku
wanajiadalia umasikini na kuishi maisha dunu tena magumu watakapo staafu wakati huu ndo wa kujipanga na maisha na kuwa
mfano wa kuingwa najamii bada ya kustaafu.
Mratibu Elimu Kata ya Namonge Alex Nkingwa alisema madai ya
walimu hao anayajuwa na kwamba yametolewa ufafanuzi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk John Magufuli baada ya kuwasilishwa na vyama mbali mbali vya
watumshi kwenye sherehe za kitaifa katika viwanja vya Samola Mkoani Iringa.
Comments
Post a Comment