SERIKALI KUTOA MASAA 72 KWA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO WALIOJENGA VIBANDA CHINI YA NYAYA ZA UMEME WA TANESCO KUONDOA

Serikali Wilayani  Bukombe Mkoa wa Geita imetowa maasa 72 kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa nafaka na matunda waliojenga vibanda chini ya nguzo za umeme wa TANESCO mtaa wa Uhamiaji Kata ya Katente Wilayani hapa kuondoa ili kupisha miundombinu hiyo.
Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Josephat Maganga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Butambala baada ya  malalamiko ya uvunjwaji wa sheria yaliyofikishwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama na halmashauri kupita idara ya ardhi pamoja na shirika la umeme Tanzania TANESCO  na kamati ikafatilia na kujiridhisha kuwa wananchi wamejenga vibanda chini ya Nguzo za umeme kwa madai kuwa wamepewa na Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Bukombe hali ambayo si kweli.
Maganga alishirikiana na watalam mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi wa Kata nne Katente,Ushirombo,Igulwa, Bulangwa,  juu ya madhara ya umeme.
Alisema kutokana na kubaini kuwa kuna uvunjaji wa sheria mkubwa uliofanywa na wafanyabiashara hao kwa kujenga vibanda chini ya nyaya za umeme zenye Msongo Kilovoti 33 baada ya kugawiwa ki holela aliwasihi kuviondoa kupisha miudo mbinu hiyo baada ya masaa 72.  
Pia alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kuharakisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili biashara ya soko yanalipwa fidia mapema tayari kwa kuwagawia wananchi hao.   Meneja wa shirika la umeme Wilaya ya Bukombe Thadey  Mapunda alisema mradi huu kwa awamu ya kwanza vitongoji na vijiji 80 vinanufaika  na kwamba sheria zinataka njia ya umeme iwe wazi na asiwepo mwananchi wa kuvamia kufanya shughuli yeyote ya kibinadamu chini ya nguzo za umeme ili kuepuka athari inayoweza kujitokeza kuaguka nguzo ama waya.
Miongoni mwa wafanyabaishara waliojenga vibanda kwenye maeneo hayo   Adam Machungwa alitupia lawama serikali kwa kuwaingiza mkenge wananchi wake kutumia ghalama kubwa kisha kuwafukuza hali ambayo inaludisha maendeleo nyuma kwa wananchi wa maisha ya chini.Machungwa alisema walipewa na viongozi wa serikali za mitaa Aprili mwaka huu waliaza kujenga vibanda,lakini serikali  hiyo hiyo inatufukuza wakati tumejenga kwa ghalama za kuuza kuku za kufuga zikiwemo bidha mbali mbali za ndani.
 Hoja hiyo iliungwa mkono na  barozi wa nyumba 10 mstafu mtaa wa Bomani  Suzana   Giti alisema waligawiwa maeneo  hayo kwa lengo la wananchi wafanye shughuli za ujasiliamali ili kujikwamua na umasikini aliomba seriakli kutowanyang’anya maeneo hayo badalayake waruhusiwe kuyaendeleza  kwa kufanyia biashara.

Comments