Morata Atupwa Nje Ya Kikosi Cha Timu Ya Taifa Hispania.

Alvaro Morata Mshambuliaji kutoka klabu ya Chelsea mwenye umri wa miaka 25, ametupwa nje ya kikoso cha timu ya Taifa ya Hispania kitakacholiwakilisha taifa hilo katika michuano ya kombe la Dunia mwezi ujao.
Morata alifunga mabao 11 msimu wake wa kwanza akiwa Stamford Bridge na alichezeshwa kama nguvu mpya dakika za mwisho mwisho wakati wa fainali ya Kombe la FA ambapo Blues walilaza Manchester United 1-0 Jumamosi.
Kikosi Cha Hispania Kilichotajwa:
Walinda lango: David de Gea (Manchester United), Pepe Reina (Napoli), Kepa Arrizabalaga (Athletic Bilbao).
Mabeki: Jordi Alba (Barcelona), Nacho Monreal (Arsenal), Alvaro Odriozola (Real Sociedad), Nacho Fernandez (Real Madrid), Dani Carvajal (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Cesar Azpilicueta (Chelsea).
Kiungo wa kati: Sergio Busquets (Barcelona), Isco (Real Madrid), Thiago Alcantara (Bayern Munich), David Silva (Manchester City), Andres Iniesta (Barcelona), Saul Niguez (Atletico Madrid), Koke (Atletico Madrid).
Washambuliaji: Marco Asensio (Real Madrid), Iago Aspas (Celta Vigo), Diego Costa (Atletico Madrid), Rodrigo Moreno (Valencia), Lucas Vazquez (Real Madrid).

Comments