MHE. BITEKO ATOA MOTISHA KWA MWANAFUNZI ALIYEFANYA VIZURI USHIROMBO SEKONDARI



 Wanafunzi wa kidato cha nne 2016 Shule ya Sekondari Ushirombo wakipokea unga,maharage na mchele ikiwa ni motisha ya chakula kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko ili wakae shuleni hapo kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa taifa (picha hii ni ya 2016)



Mwanafunzi aliyefanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza kidado cha nne mwaka 2017 shule ya Ushirombo sekondari Kata ya Bulangwa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,Bonephace Bagasa  amepokea motisha baada ya sh 100,000 na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ikiwa ni moja ya ahadi zake kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa watakao faulu.
Akizungumuza shuleni hapo baada ya kukabidhiwa mbele ya wanafunzi wa shule hiyo Bagasa alimshukuru Mbunge kwa kujitoa kuhamasisha ufaulu kwa wanafunzi na kuomba viongozi wengine waige mfano huo.
Bagasa alitoa wito kwa wanafunzi kuwa ili wafanye vizuri inawapasa kuheshimu wazazi na walimu na kuachana na makundi lika wanapokuwa shuleni na nyumbani aliwasihi kujitengea munda wa kujisomea wakiwa nyumbani na kujituma wakiwa shuleni.

Mkuu wa shule msaidizi Ushirombo Sekondari Mabula Ngela alisema mwaka 2017 wanafunzi watahiniwa walikuwa 266 wavulana walikuwa 162 wasichana 104 lakini mwanafunzi Boniphace Bagasa alifaulu kwa kupata divisheni 1peke yake.
Ngela alimpongeza na kumshukru Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko  kwa kutimiza ahadi yake aliyoitowaga shuleni hapo wakati wa mahafali ya wanafunzi hao mwaka 2017 kuwa mwanafunzi atakaye pata divisheni 1 atampa motisha hali ambayo iliawafanya wanafunzi kujituma kwenye masomo.

 Pia aliahidi kuongeza ufaulu ili kutomvumja moyo Mbunge kwa kutoa mitihani ya majaribio ya mara kwa mara kwa wanafunzi 206 ambao wako kidato cha nne mwaka 2018 .

Alisema wamejiwekea mikakati ya kudhibiti hali ya utoro ikiwa hali ya nyuma kulikuwa na utoro kwa kushirikiana na wazazi na walezi na kwamba wamekuwa wakihamasisha wanafunzi kujisomea na wazazi kuwatengea munda wakujisomea wanapokuwa nyumbani.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Benjamin Elias Mgeta akikabidhi motisha hiyo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko aliwaomba wazazi na walezi kuwekeza kwenye elimu ili kuwawezesha vijana kufanya shughuli za kujiajiri kwa ufanisi mzuri na wengine kuajiliwa na serikali pamoja na sekta mbalimbali nchini.

Mgeta aliwaomba walimu kutambua kazi yao ni ya wito hivyo wahahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa kuzingatia maadili ya utumishi na kuishi vizuri na jamii inayowazunguka.

Comments