MBUNGE AWAUNGA MKONO WANANCHI BATI 100


Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kata ya Bulangwa katika viwanja vya Kilimahewa Mjini Ushirombo ikiwa ni utaratibu wake ili kupokea na kubaini changamoto zao.
Mwenyekiti wa CCM(W)Bukombe Daniel Machongo akizungumza na wananchi wa Kata ya Bulangwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM(W)Bukombe Ladislaus Soku akizungumza na wananchi wa Kata ya Bulangwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mbuge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Mbuge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na mwenyekiti wa Kitongoji

Kutokana na wananchi kusitisha kutoa michango ya shughuli za maendeleo, Kata ya Bulangwa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita na kusababisha miradi ya miundo mbinu ya madarasa kubaki hewani Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko amechagia mabati 100 geji 28 yenye thamani ya Sh 2.6 milioni.

Mchango huo ulitolewa baada ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Bulangwa Mariko Nsolo kusoma risala na kubainisha changamoto hiyo kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Bulangwa uliokuwa umeitishwa na Mbuge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Nsolo alisema changamoto katika maeneo ya miradi ya maendeleo kusimama kutumia michango ya wananchi tangu tamko la Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli kusitisha michango na kutafasiliwa vibaya kwenye jamii mwaka 2017 hali ambayo imepelekea miradi kusimama.

Nsolo alisema kutokana na upugufu wa madarasa na ofisi ya walimu shule ya msingi Azimio kulikuwa na ujenzi wa vyumba vya madarasa 4 na ofisi 2 za walimu hadi usawa wa renta sh 7,124,000 nguvu za wananchi sh 5,624,000 serikali kuu sh 1,500,000  fedha zilizo tumka hadi sasa  7,124,000.

Mkazi wa Bulangwa Yasta Pero aliomba serikali kukamilisha majengo hayo ili wanafunzi waondokane na kuendelea kubanana kwenye vyumba vya madarasa

Diwani wa kata ya Bulangwa Yusuph Mohamed alimshukuru Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) kwa jitihada zake alizozionyesha kwa Kata hiyo kwa kuongeza vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Ushirombo,kutafuta fedha kwa ajili ya upanuzi wa shule ya sekondari Businda ili iwe na kidato cha tano na sita,ukarabati na upanuzi wa Kituo cha Afya Ushirombo na kuongeza mtandao wa barabara utakaokuwa una hudumiwa na TANROADS pamoja na barabara za mitaa na akuwaomba wananchi kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo ili kukamilisha miradi ambayo imesimama.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko aliwapa pole wananchi wanao tafasili vibaya tamko la Rais John Magufuli kusitisha michango iliyokuwa inaendelea kwa wazazi na walezi mashuleni hali ambayo ilikuwa inapelekea wanafunzi kurudishwa nyumbani.

Biteko alichangia bati 100 kwa lengo la kuwa unga mkono wananchi na kuwasisitiza waendelee kuchangia nguvu kazi na mali zao kwa kupitia mikutano ya serikali za vijiji.





Comments