Mbunge wa Jimbo la
Bukombe na Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amezungumza na Wenyeviti,Makatibu
na Makatibu Wenezi wa Kata zote za Wilaya ya Bukombe kwenye kikao cha kazi
kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Bukombe.
Akizungumza na Wajumbe hao alianza kwa
kuwapongoza kwa kuchaguliwa kwao na kuwaomba wasimamie katika kuhakikisha
wanamaliza makundi ndani ya chama yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi kwa
kuimarisha upendo na mshikamano baina yao sambamba na kuwaomba wazidi kuunga
mkono Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli
dhidi ya utetezi wake kwa wananchi wanyonge wenye kipato cha chini.
Pia aliwasisitiza viongozi
hao wa chama kushirikiana na watumishi wa serikali katika kuhakikisha Ilani
ya chama cha mapinduzi inatekelezwa kikamilifu huku akibainisha miradi
iliyotekelezwa Wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vituo vya Afya
huku vilivyopo vikiboreshwa na kupanuliwa,Mradi wa umeme vijijini (REA)
kusambaza vijiji vyote Wilayani humo,kutatua changamoto ya maji kwa kuanzisha miradi midogo ya
maji,ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mabalimbali ikiwemo Ibamba na Namonge
kwa shule za msingi,vyumba sita vya madarasa Ushirombo sekondari, mitandao ya barabara kuongezwa hadi kilomita 1500
na kuwa ya pili kwa Mkoa wa Geita kwa kuwa na mtandao wa barabara nyingi.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM (W)Bukombe Daniel Machongo aliwapongeza wajumbe
kwa mahudhurio yao na kuwaomba wajitume kikamilifu kukijenga na kulinda chama
hicho ili kiweze kuwa na serikali imara.
Comments
Post a Comment