
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Makamba amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali pamoja na wawekezaji inafanyiwa tathmini hiyo ili kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
“Nawapongeza WWF kwa kazi nzuri za tafiti wanazofanya na hata kupatikana kwa muongozo huu ni matokeo ya kazi nzuri waliyofanya kama wadau wetu ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira,” Alisisitiza Mhe. Makamba.
Akifafanua amesema kuwa anazikumbusha Wizara, Taasisi na wadau wote wanaotaka kutekeleza miradi ya maendeelo kuhakikisha kuwa wanazingatia muongozo huo ambao umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inajenga uchumi wa viwanda
Comments
Post a Comment