AZAM YAIANGAMIZA YANGA 3-1,WANYAKUA NAFASI YA PILI



TIMU ya Azam kimelipiza kisasi kwa Yanga baada ya kuichapa mabao 3-1 leo katika mchezo kuhitimisha mechi za ligi kuu msimu huu uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Timu hizo mbili zilikuwa zinapambana kuwania nafasi ya pili ambapo Azam wamefanikiwa kutokana na ushindi huo.Mabao ya Azam yametiwa kimiani na Yahya Zayd mnamo dakika ya 4, Shaaban Idd (60′) na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (68′).
Azam walijifunga na kuipa Yanga bao la kufutia machozi mnamo dakika ya 49 kupitia kwa Abdallah Kheri (49′) kwa kichwa wakati akifanya harakati za kuokoa mpira.Matokeo hayo yanaifanya Azam kulipiza kisasi baada ya kfungwa mzunguko wa kwanza kwenye dimba la Azam Complex kwa jumla ya mabao 2-0.
Vilvie Azam wamechukua nafasi ya Umakamu Bingwa kwa kufikisha alama 58 huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikijikusanyia pointi 52.

Comments