Yanga yafunguka kuhusu kuondoka kwa Lwandamina

Baada ya kuenea kwa uvumi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amerejea kwao Zambia kujiunga na timu yake ya zamani, Zesco United, uongozi Yanga umekiri uwepo wa taarifa hizo.

Kupitia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, Salum Mkemi, amesema kuwa ni kweli taarifa hizo zimesambaa mitandaoni lakini hawana uhakika kama Lwandamina aeshajiunga na Zesco United.

Licha ya uwepo wa taarifa hizo, Kupitia Radio EFM (E Sports), Mkemi amwemwelezea Kocha Lwandamina kama Mwalimu aliyekuwa anakuza vipaji vya vijana na kuwatengeneza kuwa mhimili wa timu.

Taarifa zilitoka hivi punde kutoka Zesco United, zimethibitisha kuwa Lwandamina ameshajiunga tayari na miamba hao wa Zambia.

Lwandamina ameondoka Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Comments