WATU 602 WAPIMA UKIMWI KWA HIYARI




Watu 602 Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wamejitokeza kujua afya zao kwa kupima kwa hiyari  VVU kati yao wanaume 413  wanawake 189  kati hao waliokutwa na maambukizi ya VVU ni 26 sawa na asilimia 12 ya maabukizi ya UKIMWI ikiwa wanawake 12  wanaume 14.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru na wakimbiza mwenge 2018 kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaban Ntarambe katika viwanja vya Kijiji cha Nyarututu Kata ya Bwanga Wilaya ya Chato.

Maganga alisema kutoka Uyovu hadi eneo la kukabidhi mwenge wa uhuru ulikimbizwa kilomita 45 aliwapongeza wananchi kujitokeza kupima VVU na kuchangia damu kwa hiyari kwenye mkesha wa mwenge wa uhuru Kata ya Uyovu wananchi walichangia kwa hiyari chupa za damu 19.

Maganga alisema  mwenge wa uhuru Wilaya ya Bukombe umegharimu Sh Sh21,577.50 kutoka kwa wadau wa maendeleo, wananchi,  halmashauri ya Wilaya  na serikali kuu, fedha hizo zimefanikisha shughuli mbalimbali za mwenge ikiwemo chakula,vinywaji, ujenzi,mapambo,Burudani, hamasa na usafiri.


Maganga  akizungumuza kwa niamba ya wananchi wa Wilaya ya Bukombe alisema mwenge wa uhuru ulikimbizwa kilomita 85 na kupitia miradi ya maendeleo 8  mmoja wa kuwekewa jiwe la msingi,  mwingine mmoja wa kufunguliwa, miradi miwili ya kuzindua,  miradi mingine minne ya kuona na kufunguliwa yenye thamani ya Sh1,154,811,623.40.
Alichanganua kuwa Nguvu za wananchi Sh 73.204 milioni halmashauri sh 8.763 milioni wahisani sh316.740 milioni serikali kuu sh 810.77 milioni.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Charles Kabeho aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Bukombe na viongozi wa serikali na wamadhehebu ya dini na kuwataka kuendelea kuwekeza kwenye Elimu na kutambua afya kwa kupima kwa hiyari na kama mtu amepatikana na maambukizi ya UKIMWI kwa bahati mbaya atumie dawa za kufubaza virusi na akizingatia ushauri wa madaktari ili aendelee kufanya kazi zake vizuri zikiwemo za uzalishaji mali.

Comments