WANAUME WILAYANI BUKOMBE WAASWA KUACHANA NA IMANI POTOFU YA MADAI KUWA VYANDARUA VINAMALIZA NGUVU ZA KIUME
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya
Iyogelo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Kabeho amewaomba wanaume kuachana na dhana
potofu ambazo hazina ukweli wowote hali ambayo imekuwa ikiwasababishia familia
nyingi kuugua maralia na kusababisha watu wasifanye kazi za kuingiza pato la
familia na taifa kwa kwenda kutafuta huduma za afya kwa ajili ya matibabu.
”acheni mila potofu za madai kuwa mwanaume akilala kwenye
kitanda chenye chandarua atapunguza nguvu za kiume si kweli niupotoshaji mkubwa
wa jamii Mungu akiwa amekuumba na nguvu za kiume za kutosha hata kama ungelala
kwenye chandarua hazitapunguwa hata kidogo tumieni chandarua safi na kusafisha mazingira yanayozunguka makazi ya nyumba ili
kuepuka ugonjwa wa maralia”alisema Kabeho.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho alitowa wito huo baada ya kupokea taarifa hiyo
kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dk Irene Mkerebe wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za
mwenge kitaifa walipokuwa wakifanya zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa baadhi ya
Wamama wajawazito na wanao nyonyesha kwenye Zahanati ya Kijiji cha Iyogeyo Kata ya Iyogelo
Wilayani Bukombe.
Dk Mkerebe alisema mwitikio wa wananchi uko chini kutokana na wanaume kuto tumia vyandarua
kitandani kwa madai kuwa vina maliza nguvu za kiume kuzalisha wadudu aina ya
kunguni.
Dk Mkerebe alisema lakini wananchi wamekuwa wakishirikishwa
kwa kupewa Elimu ya kutumia vyandarua na tayali wamegawa kuanzia februari 2017 hadi
februari 2018 vyandarua 26,357 kwa wanafunzi
wa shule za msingi, 204,744 kwa akinama
wajawazito na vyandarua 11,005 vimegawiwa kwa watoto wanao ugua surua na vyandarua
`170,225 kwa wananchi ikiwa ni lengo la kutekeleza
mikakati ya kupambana na mbu waenezao maralia,kutoa Elimu dhidi ya maralia,
ufatiliaji wa mabadiliko ya hali ya hewa ya mbu waenezao maralia kwenye vijiji
viwili vinavyo vinaongoza kwa mbu wengi ambavyo ni Sinamila Kata ya Nganzo na Kijiji
cha Imalamagigo Kata ya Igulwa.
Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe Josephat Maganga wakati akipokea mwenge wa uhuru na kuzungumuza kwa
niamba ya wananchi wa Wilaya ya Bukombe katika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Bugelenga
alisema Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Bukombe utakimbizwa kilomita 123 na kupitia miradi ya maendeleo
8 mmoja wa kuwekewa jiwe la msingi, mwingine mmoja wa kufunguliwa, miradi miwili
ya kuzinduwa, miradi mingine minne ya kuona
na kufunguliwa yenye thamani ya Sh1,154,811,623.40.
Pia Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Kabeho akihutubia wakazi
wa kata ya Uyovu ulipo lala mwenge aliwakumbusha wananchi,wazazi na walezi
kuwekeza watoto wao kwenye Elimu na kuwalea watoto kwenye misingi ya maadili
mazuri na kuwanusulu vijana katika utumiaji wa madawa ya kulevya huku akisisitiza
kupigana na adui wa haki, Rushwa kwa kutoa taarifa TAKUKURU wakati wananchi
wanatafuta huduma kwenye ofisi yeyote na kuombwa rushwa na kuepukana na maambukizi
mapya ya UKIMWI.

Comments
Post a Comment