Vilabu 16 Vilivyofuzu Katika Hatua Ya Makundi, Vitano Kutoka Afrika Mashariki Na Kati.

Jumla ya vilabu vitano kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati vimefuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho la soka barani Afrika baada ya michuano ya mtoano kumalizika siku ya Alhamisi.
Vlabu hivyo ni pamoja na Al Hilal ya Sudan, AS Vita Club ya DRC, Yanga ya Tanzania, Gor Mahia ya Kenya na Rayon Sports ya Rwanda.
Kwa upande wa Yanga licha ya kufungwa bao 1-0 na Welayta Dicha ya Ethiopia, ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 uliwasaidia kufuzu katika hatua hiyo.
Nayo Gor Mahia ya Kenya ambayo imeweka historia kwa kufuzu katka hatua hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya miaka 31 iliposhinda taji la Afrika, licha ya kufungwa na SuperSport United mabao 2-1 ugenini, ushindi wao wa bao 1-0 uliwasaidia.
Mambo yalikuwa mazuri pia kwa Rayon Sport ya Rwanda ambayo licha ya kupoteza kwa mabao 2-0 baada ya kufungwa na Costa do Sol ya Msumbiji, ushindi wake wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ulitosha kuwasaidia.
Vlabu 16 zimefuzu katika hatua ya makundi, na sasa droo itafanyika siku ya Jumamosi ambapo kutakuwa na makundi manne, kila kundi na vilabu vinne.

Comments