Trump aahidi kujibu mapigo shambulio la douma Syria

Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kutumia nguvu kujibu madai ya shambulio la kemikali nchini Syria, huku mataifa ya magharibi yakitafakari hatua watakayoichukua.

Rais Trump amesema kuwa hatua ya kujibu shambulio hilo itaamuliwa katika kipidi cha muda mfupi na kwamba Marekani ina njia nyingi za kijeshi kujibu shambulio hilo.

Aongeza kuwa Marekani iimepata taafia za uhakika juu ya nani aliyehusika na shambulio la mjini Douma lililotokea Jumamosi iliyopita nchini Syria.

Habari zanasema kwamba watu zaidi ya 50 waliuawa katika shambulio hilo wakiwemo wanawake na watoto.

Kauli za viongozi wa kimagharibi za kulaani shambulio hilo zimefuatia kikao cha malumbano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo Marekani na Urusi walitupia na maneno makali kuhusiana na tukio la Douma.

Comments