Wanafunzi wa Sekondari zaidi ya 300 Kata ya Busonzo Tarafa ya Siloka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wanalazimika kutembea umbali
mrefu zaidi ya kilomita 18 kutokana na ukosefu wa shule ya sekondari kwenye Kata hiyo wanafunzi wamekuwa wakienda Kata jirani ya Uyovu hali ambayo imekuwa
ikipelekea wanafunzi wengi kukata tamaa na kushindwa kuhitimu kidato cha Nne. 
Mratibu Elimu Kata ya Busonzo Ramadhan Mngoi aliyasema hayo
wakati wa ziara ya Mbunge Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko alipo kuwa kwenye ziara Kata
ya Busonzo Aprili 2 mwaka huu kwa lengo la kujuwa changamoto zinazo pelekea
wanafunzi kutembea umbali mrefu na mradi wa shule ya Busonzo sekondari
kushindwa kukamilika tangu mwaka 2012.
Mngoi alisema Kata ya
Busonzo ina shule za msingi tano zinafaulisha wanafunzi kujiunga na sekondari
kila mwaka lakini tangu 2012 hadi mwaka 2017 wanafunzi zaidi 300 wanatembea
umbali mrefu kutoka kijiji cha Namparahala kata ya Busonzo kwenda Kata
jirani ya Uyovu kwenye shuleni ya Runzewe sekondari wanatembea kilomita zaidi
ya 18 kati ya wanafunzi hao hutoka vijiji vya mbali zaidi.
Mngoi alisema kutokana na umbali huo wanafunzi wamekuwa
wakifauru kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza lakini wanashindwa kufikia
ndoto zao za kumaliza kidato cha nne kutokana na wengi wao kukata tamaa kwa kutembea
umbali mrefu.
Alisema mwaka 2018 pekee wanafunzi walio anza kidato cha kwanza
kutoka Kata ya Busonzo kwenda Kata jirani ya Uyovu ni zaidi ya wanafunzi 122 wanatembea
kwa mingu na wengine kwa baiskeli na wazazi wengi wamekuwa wakishindwa
kuwapangishia vyumba karibu na shule ya Runzewe sekondari kwa kwa madai kuwa
wanashindwa kumundu gharama za kuwahudumia kama sehemu ya familia hali ambayo
inapelekea wanafunzi hao kukata tamaa huku walioanza kidato cha kwanza ni wanafunzi 122 wanahitimu kidato cha nne
wanafunzi 30 wengi wao kuishia kuolewa na kuowa na kufanya biashara.
Mngoi alisema shule ya Runzewe sekondari imeadikisha zaidi ya
wanafunzi 500 wakati uwenzo wa shule hiyo ni mdogo iwapo shule ya Busonzo
sekondari itakapo kamilika na kufunguliwa matarajio mwenzi Junu mwaka huu itasaidia
kupunguza msongamano wa wanafunzi Runzewe sekondari na kwamba kuna madarasa 4 nyumba
ya mwalimu moja matundu 10 ya choo
wanafunzi, matundu 2 ya choo cha walimu kuna ujenzi wa maabara vyumba vitatu.
Mayala aliwaomba wananchi kuwa tayali kuchangia miradi ya
maendeleo wakati wa miradi inapo anzishwa ili kuondoa changamoto zinazo
wakabili wananchi ili waondokane na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya
na wanafunzi kufata Elimu kata jirani.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko wakati wa ziara yake ya
kuhamasisha maendeleo Kata ya Busonzo Aprili 2 mwaka huu ambapo zaidi ya
miaka mradi wa ujenzi wa shule ya Busonzo Sekondari umeshindikana kukamilika kutokana na wananchi kujikita kwenye mambo
ya kisiasa na kutoa changia maendeleo.
Biteko akiwa kwenye mkutano wa hadhara akipokea taarifa ya
utekelezaji wa mradi huku aliiomba serikali
na imetoa sh 40 milioni kupitia mfuko wa
P4R kuongeza nguvu kuhakikisha shule hiyo inafunguliwa na kuchagia tofari
10,000 za choma zenye thamani ya million moja na laki mbili ambazo alizielekeza
kukamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara vitatu ili wanafunzi waondokane na changamoto
ya kutembea umbali mrefu kutafuta Elimu Kata jirani ya Uyovu.
Biteko aliwaomba wananchi kuvuja makundi ya kisasa na kuwaunga mkono viongozi
ambao wamechaguliwa na wananchi kwa kupingiwa kura na wengine kuajiliwa na serikali pamoja na
kuwaelimisha wananchi madhara ya kuendekeza siasa wakati uchaguzi umekwisha hali
ambayo inakwamisha maendeleo na kuwapa mzingo wananchi ambao wanahitaji
kusogezewa huduma za kijamii.
Comments
Post a Comment