WILAYA YA BUKOMBE YATOA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA UZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 14



Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, kupitia mpango wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi mwaka 2018/19 wasichana  2800 wenye umri wa miaka 14 watafikiwa kupewa chanjo hiyo ikiwa wengi wao ni wanafunzi shule za msingi na sekondari pia chanjo itatolewa kwa wasichana ambao hawasomi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji.
Aliyasema hayo  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dk Irene Bukerebe kwenye uzinduzi wa kiwilaya wa wiki ya Chanjo ya kuzuia sataratani ya mlango wa kizazi kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Ushirombo Kata ya Bulangwa  katika uzinduzi huo wasichana 124 wenye umri wa miaka 14 walichanjwa chanjo hiyo ikiwa malengo ya halmashauri hiyo nikuwafikia wasichana 2800 kwa mwaka 2018/19.
Dk Bukerebe alisema mwaka 2017 takwimu ya wanawake 1700 wenye umri wa miaka 30 hadi 50 walihamasishwa kupima kwa hiyali saratani ya mlango wa kizazi katika hospitali ya Wilaya kati yao 147 walikutwa na dalili za ugonjwa huo na waliazishiwa matibabu huku miongoni mwao wanawake 17 walikutwa na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi, na kulazimika kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.
Miongoni mwawanafunzi walio patiwa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi toka shule ya msingi Kapera darasa la saba Agnes Ezekiel alisema chanjo hiyo itamsaidia kujikinga na magonjwa huku akiwaomba wanafunzi wezake kuacha tabia ya kujiingiza kwenye dimbwi la mapenzi wakawa na umri mdogo.
 Nae Diwani wa Kata ya Bulangwa Mhe. Yusuph Mohamed aliiomba serikali kuwachukulia hatua wazazi watakao bainika wamewakataza watoto wao kupatia chanjo kwa kuamini mila potofu hali ambayo huendeleza kuunda jamii ya wasiojitambua.   
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akiwahutubia wananchi katika uzinduzi huo aliwaomba wazazi na walezi kuachana na mila potofu kwenye chanjo zinazotolewa na serikali kupitia watalamu wa Afya badalayake wazazi wawaruhusu watoto wao wakapewe chanjo ya ugonjwa huo ili wasije wakakubwa na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi, au vifo visivyo vya lazima.
Aliagiza serikali za vijiji kuzitambua kaya zenye wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao hawasomi ili nao wapatiwe chanjo mara tu  watalamu wa afya watakopo kuwa wanapita kutoa huduma ya chanjo ya kuzuia saratani ya  mlango wa kizazi mashuleni na vijijini kwenye ofisi za serikali, "lengo la serikali nikukinga magonjwa na kuwa na taifa lenye wanawake bora wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali kuanzia ngazi ya familia hadi taifa."Maganga alisema
Pia Maganga alitowa wito kwa wanasichana wenye umri wa miaka 9 na 14 kutojihusisha na mapenzi wakawa wa umri mdogo na kuwasisitiza kuwa ni chanzo cha kupata ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi huku akiwaomba wazazi na walezi kuwaelimisha watoto wao ili wazingatie maadili ili kuepukana na maradhi pamoja na mimba za utotoni  zinazojitokeza mara kwa mara katika jamii.

Comments