Chunga Sana Matumizi Haya Ya Pesa Ili Yasikupoteze


Kitu cha msingi unachotakiwa kuzingatia wakati unatumia pesa zako, ni ubora wa vile vitu ambavyo unakwenda kuvipata wakati unatumia pesa zako.

Kama unatumia pesa zako kwa vile vitu ambavyo viko bora wakati wote, basi pesa zako wakati wote ziko salama na zitakusadia kupiga hatua ya aina fulani.

Kama unatumia pesa zako kwa mambo ya hovyo hovyo basi hata kama kipato chako ni kikubwa kiasi gani, pesa hizo utakuwa unazipoteza tu bure na hakuna unachofaidi.

Wakati wote unatakiwa kuzingatia ni kwa namna gani unafanya matumizi yako kwa ubora, ikiwa unafanya matumizi yako kwa ubora utajiweka kwenye wakati bora pia.

Watu wengi wanajikuta wameishia na hawana kitu kwa sababu ya kufanya matumizi yasiyo ya msingi, bali wanafanya matumizi ya kuwabomoa.

Kila wakati chunga matumizi yako na hakikisha unajua pesa zako zinakwenda wapi kila siku iitwapo leo.

Kutumia zako hovyo, huko ni kujitakia majanga yaw ewe kuweza kuishia kwa baade. Tumia pesa zako kwa busara nazo pia zitakulinda

Comments