WADAU WA ELIMU WACHANGIA UJENZI WA SEKONDARI KATA YA IGULWA -BUKOMBE




Wadau wa maendeleo ya elimu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,
wamechagia Tsh miloni nne kwa ajili ya kupauwa shule ya  Sekondari Igulwa
kwa kuwaunga  mkono wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya wadau hao Sang'udi alisema watahakikisha
wanashirikiana na wananchi walionazisha miradi ya maendeleo kikamilifu kusukuma gurudumu hilo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Igulwa Gaudensia Dalali akisoma risara ya
ujenzi wa sekondari alisema ujenzi uliaza mwaka 2017 hadi kukamilika
utagarimu sh 87,760,000 nguvu za wananchi  mpaka sasa wamechangia Tsh
 milioni11  lengo ifikapo Julai 2018 shule iaze kutumika.

Dalali aliongeza kuwa ukusanyaji wa michango kwa wananchi ulianza
Julai 1 mwaka 2017 na mwisho Oktoba 30 mwaka 2017 watu 10,000 ndiyo
kila mmoja anatakiwa kuchangia sh 3,000 katika mchango huo ikiwa watu ambao hawaja changia ni 6,333 sawa na Tsh 18,999,000.

Dalali alitaja changamoto zilizo jitokeza wakati wakiendesha msako wa
mchango huo ikiwa ni pamoja na wanasiasa ambao walikuwa wanapotosha wananchi kuhusu
tamko la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuhusiana na michango ya hiyari hali ambayo ilipelekea watu kupunguza kasi ya uchangiaji huku wengine kudai
michango yao walikwisha kuitoa.

Alisema kutokana na wanasiasa uchwara kupotosha wananchi kuchangia
kiasi hicho cha fedha hivyo kupelekea madeni makubwa wanayodaaiwa
yakiwemo ya vifaa  vya ujenzi  na mafundi ambao ni Local fundi na
mabati 200 yenye thamani ya Tsh milioni 6.7 kwa ajili upauji wa jengo hilo.

Upande wake Afisa elimu Sekondari Wilaya ya Bukombe Philibert
Nyangahondi alisema Wilaya ya Bukombe ina Kata 17 na mahitaji ya shule za sekondari
ni 17 zilizopo 14 upungufu shule 3 na kuwaomba wananchi kushikamana na
viongozi wa serikali ili kufikia malengo ya maendeleo.

Nyangahondi alisema iwapo shule ya sekondari ya Igulwa itakamilika
itapunguza msongamao wa wanafunzi kwenye shule za sekondari za
Businda,Ushirombo,Katente ambapo wanafunzi wengi kutoka kata ya Igulwa
hutembea umbali mrefu kwenda katika shule hizo za jirani.

Mbuge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko wakati wa ziara  ya kwenda anasikiliza kero za wananchi na kuwahimiza
kuchangia miradi ya ujenzi wa Zahanati Vituo vya Afya na shule za
msingi na sekondari aliwaomba wananchi kupuuza upotoshaji wa wanasiasa
uchwara wanaofanya upotoshaji kwa wananchi kuwa wasichangie michango
ya hiari kwa madai eti  serikali italeta fedha kwa ajili ya ujenzi.

Biteko alisema kutokana na wananchi wa Igulwa kuanzisha ujenzi wa
vyumba vitano vya shule ya sekondari na kufikia usawa wa renta
alichangia sh2.7 milioni na kuwapongeza wadau wa elimu Wilayani hapa
kwa kuchangia sh 4 milioni kwa kuwaunga mkono wananchi ili wapate
mabati ya kutosha kuezeka shule hiyo.

Mbunge aliwaomba viongozi wa naounda Kamati ya maendeleo ya Kata kuhamasisha wananchi kuendelea kujitolea kwa hiari yao kuchangia kwa hari na mali ili kuhakikisha wanaanzisha na wanamalizia ujenzi wa maabara na nyumba za walimu ili kuondoa changamoto zitakazo jitokeza pindi shule itakapoanza.


Comments