Naibu Waziri wa Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasitiza waumini waliohudhiria kwenye ibada ya jumapili katika kanisa la EAGT lililopo katika kijiji cha Dyobahika, Kata ya Uyovu, Wilayani Bukombe Leo 4 Machi 2018 wakati akitoa salamu za serikali.
Mbele ya waumini wa kanisa la EAGT lililopo katika kijiji cha Dyobahika, Kata ya Uyovu, Wilayani Bukombe, Naibu Waziri wa Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasihi waumini waliohudhiria kwenye ibada ya jumapili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, Leo 4 Machi 2018.
Naibu Waziri wa
Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko
(Kulia), Katibu wa Mbunge huyo katika jimbo la Bukombe Elius Benjamin
Mgeta (Katikati), na Katibu wa Naibu Waziri huyo Mhandisi Kunguru
Kasongi wakifatilia mahubiri katika kanisa la EAGT lililopo katika kijiji cha Dyobahika, Kata ya Uyovu, Wilayani Bukombe, Leo 4 Machi 2018.
Mbele ya waumini wa kanisa la EAGT lililopo katika kijiji cha Dyobahika, Kata ya Uyovu, Wilayani Bukombe, Naibu Waziri wa Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasihi waumini waliohudhiria kwenye ibada ya jumapili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, Leo 4 Machi 2018.
Ni miaka
miwili sasa na ushee imepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aingie madarakani tarehe 5 Novemba mwaka 2015,
ambapo mpaka sasa kuna mambo mengi ameyafanya ambayo ni moja ya sehemu za ahadi
zake alizoahidi alipokuwa akiinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kampeni
za uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Miongoni mwa mambo msingi kabisa katika serikali ya awamu ya
tano ni pamoja na uwajibikaji wa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla kwani
kumekuwepo na ari ya kufanya kazi kwa bidii na
weledi mkubwa, umakini wa wananchi katika ulipaji wa kodi, vita ya ufisadi
imekuwa kubwa na imesaidia kuleta mageuzi na fedha ambazo zimekuwa zikiokolewa
kutokana na vita hiyo zinaelekezwa kwa wananchi kupitia miradi ya
maendeleo, Kuongezeka maradufu kwa ukusanyaji wa mapato kutoka
Sh 9.9 trilioni kwa mwaka hadi Sh14 trilioni kwa mwaka.
Naibu Waziri wa
Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko amebainisha
hayo Leo 4 Machi 2018 wakati akitoa salamu za serikali kwenye ibada ya jumapili
katika kanisa la EAGT lililopo katika kijiji cha Dyobahika, Kata ya Uyovu,
Wilayani Bukombe.
Mbele ya waumini
hao Mhe Biteko alisema kuwa mambo mengine muhimu yaliyofanywa na Rais Magufuli
ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa kama
vile ujenzi wa reli ya kisasa na uboreshaji wa shirika la ndege, Katika sekta ya kilimo serikali ya Rais
Magufuli imeondoa Tozo na Kodi nyingi zilizokuwa kero kwa watanzania ikiwa ni
pamoja na elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya awali mpaka
sekondari.
Aliongeza kuwa serikali inapigania kwa makusudi
makubwa kabisa rasilimali za Taifa, ambapo vita katika eneo la
madini ilipelekea kupitia upya mikataba yote ya uwekezaji jambo ambalo
limefanya kujitambua kama Taifa lenye rasilimali nyingi na muhimu hatimaye sasa
wawekezaji wanajua Tanzania ukienda lazima uheshimu sheria na taratibu za nchi
katika uwekezaji na uchimbaji wa madini.
Biteko alisema katika miaka
ya nyuma wawekezaji wa kigeni walitumia vibaya rasilimali za Taifa ambapo
katika sekta ya Madini walichimba Madini mbalimbali nchini pasina kunufaisha
watanzania waliondoka nayo na kunufaisha mataifa watokayo.
Aliwaeleza waumini hao kuwa
jukumu lao kuu kwa sasa ni kuiamini serikali inayoongozwa na Rais Magufuli
lakini jambo la pili ni kuiombea serikali nzima ili kutimiza wajibu wake kwa
watanzania kwa haki pasina upendeleo.
"Ndugu zangu naomba
niwaambie ukweli kabisa kuna watu wanasema hawamuelewi Rais wetu, yawezekana
haeleweki kwa kuwa anasimamia haki kwa ajili ya wananchi wanyonge na kuwatoa
katika maisha ya mazoea waliyoishi katika kipindi kirefu na kuyageuza ndio
utaratibu" Alikaririwa Biteko (Mb) huku akishangiliwa na mamia ya waumini
hao
Katika hatua nyingine Mhe
Biteko amekemea vikali siasa zinazorudisha nyuma maendeleo badala yake
amewataka wanasiasa wenzake kuhubiri kweli na siasa yenye tija ya maendeleo kwa
wananchi.
Comments
Post a Comment