Wanakwaya wa Kanisa la Wadventista Wasabato Maganzo wakitoa mahubiri kwa njia ya nyimbo.
Waumini
Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lameck Warangi ambae pia ni muumini wa Kanisa hilo akizungumza na Waumini wenzakeNaibu wa Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa amejumuika na viongozi pamoja na waumuni wa Kanisa la Wadventisti Wasabato- Maganzo kuwaombea viongozi wa serikali ya awamu ya tano waendelee kuchapa kazi.
Waumini wa madhehebu mbali mbali ya kidini wametakiwa
kuendelea kuchangia maaendeleo ya kanisa na miradi ya maendeleo inayoibuliwa
kwenye vijiji wanako toka.
Rai hiyo ilitolewa na
Naibu waziri wa madini pia Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko wakati akijibu risala ililohitaji mchango wa Tsh milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya
mziki vya kisasa vya kanisa la Waadventista
Wasabato Maganzo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Biteko alichangia Tsh milioni mbili hali ambayo ilipelekea Mbunge
kuendesha harambe kanisani hapo na kukusanya fedha milioni 4.6 ambapo keshi ilipatika Tsh milioni mbili huku
zingine zikitolewa ahadi za viongozi wa
kanisa hilo.
Awali mwenyekiti wa kinamama kanisani hapo Savera Mandago
alisema kuwa waumini wa kanisa hilo wanafuraha ya kuabudu pamoja na Naibu
Waziri wa Madini pia Mbunge wao nakwamba kanisa la Maganzo nikituo kikuu cha
Makanisa ya Wasabato Wilaya ya Bukombe jumla ya washirika waumini 918 kutokana na changamoto ambayo wamekuwa
wakiipata wakati wa makambi wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vyombo vya
mziki.
Mandago kupitia risala alimuomba Naibu Waziri wa madini
kuchangia TSh milioni 10 ili wanunuwe
vyombo vya mziki wa kisasa ambao utawarahisishia kuendeleza kazi ya Mungu.
Mkurugenzi wa shule ya Emink sekondari Emmanuel Kalamu akiahidi Sh 700,000 aliutupia
lawama uongozi wa kanisa hilo katika mwaliko wake hakuadaliwa kuwa kutakuwa na
changizo hali ambayo agejianda vizuri badara ya kiasi hicho alicho tamuka.
Mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato Maganzo Mch. Godwin Lazaro akishukuru wageni waalikwa
na kuchangia mali zao kuwezesha kazi ya Mungu alisema wataendelea kumuunga mkono
Naibu Waziri wa Madini kwenye Jimbo la Bukombe katika kuchangia shughuli za
maendeleo nje ya kanisa na kanisani ili kufikia malengo.
Comments
Post a Comment