Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Bukombe Mkoani Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko amekutana na wafugaji wa Kata ya Iyogelo na kuzungumza nao huku akiwasisitiza
wazingatie agizo la serikali kuondoa ng’ombe ndani ya hifadhi ya kigosi Muyowosi
na kuanzisha ufugaji wa kisasa
Biteko alitoa tamko hilo wakati akizungumuza na wafugaji wa
ng’ombe kata ya Iyogelo walipo muomba aishawishi serikali kuwakatia sehemu ya
marisho kwenye pori la akiba linalo pakana na Wilaya ya Bukombe.
Naibu Waziri wa Madini Biteko wakati wa ziara yake ya kwenda
anasikiliza kero za wananchi Jimboni kwake, wafugaji amewambia kuwa hawezi
kwenda kushawishi serikali kuvuja sheria ya kuhifadhi mapori ya akiba nchini
yaliyo tengwa kisheria na kuwasihi nao wahusike kuitunza lasilimali ya taifa kwa faida ya vizazi vijavyo.
“nilichokiona kwa wafugaji wa Kata ya Iyogelo wanataka
marisho, na kuna manyanyaso kati ya askari wa wanyamapori na wafugaji,pia wafugaji wenyewe kwa wenyewe kugeukana na
kucholeana dili kwa askari wa wanyamapori, kibaya zaidi wananchi wakawaida kujifanya
askari wa wanyama pori swala la pori
kukatwa kwa ajili ya marisho haitawezekana kwa sasa lakini wananchi naomba kueni na uvumilivu “alisema
Biteko.
Alisema serikali inajipanga kutatua kero za wafugaji ndio maana
imeelekeza ngombe wa watanzania wapigwe chapa na kuwaomba wafugaji kubadilika
kulingana na mabadiliko ya nyakati viongozi wa serikali zilizopita
hawakusimamia sheria ndio maana wafugaji hao walijijengea tabia ya kuchungia mifugo ndani ya hifadhi na kuongeza kuwa
asilimia 80 ya ardhi Wilaya ya Bukombe ni hifadhi asilimia 20 ni kwa ajili ya
makazi, kilimo, na shughuli mbali mbali za kibinadamu.
Biteko aliwaomba wafugaji kupunguza mifungo yao badara ya
kuwa na ng’ombe 1000 wauze wabakize 10 na wazifuge kisasa ili kwendana na
maelekezo ya serikali na kuacha tabia ya kuomba serikali kukata pori kwa ajili
ya marisho.
Miongoni mwa wafugaji Luziri Abeli alimuomba Naibu Naziri wa Madini kuwa afatilie ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni yake 2015
kuwa wampigie kura atawategea maeneo ya marisho hoja hiyo iliungwa mkono na
mfugaji Lucas Elias nakuongeza kuwa serikali ione umuhimu wa kutenga eneo ndani
ya hifadhi wafugaji wako tayali kulipia kila mwezi hali ambayo itaongeza pato
la taifa.
Ofisa mifungo Kata ya Iyogelo Aroyce Mbulamatale alimpongeza Naibu Waziri wa Madini ambae ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa kusimamia sheria
za nchi na kwamba Kata ya Iyogelo inang’ombe 5.017 na tayali wamepigwa chapa
kufuatia angizo la serikali ili kutambua mifungo ya wafugaji wa kitanzania ili serikali
itowe huduma kwa wananchi jamii ya wafugaji na kuwasihi wananchi hao kuwa na subira wakati serikali ikifanya mchakato wa kuwatengea maeneo kuliko kuvunja sheria kwa kuwapoleka mifugo tena katika pori la akiba na kujikuta wanawajibishwa kisheria ikiwemo kufirisiwa mifugo yao.
Comments
Post a Comment