Mvua Inayoendelea Kunyesha Kenya, Yaua 15.


Jumla ya watu 15 wameripotiwa kupoteza maisha nchini Kenya kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Ripoti zinasema kwa muda wa siku mbili zilizopita, mvua hiyo ilisababisha mafuriko makubwa jijini Nairobi na maeneo mengine ya nchi hiyo. Wakenya wamekuwa wakihesabu hasara na kuomboleza vifo vya watu hao waliosombwa na maji katika Kaunti za Nairobi, Pwani, Mashariki na Kaskazini Mashariki. Miili ya watu wanne, imepatikana katika mto Athi pembezoni mwa barabara kuu kutoka jiji kuu Nairobi kwenda Kangundo.
Mafuriko makubwa yaliyotokea baada ya mvua ya siku ya Alhamisi, yamesababisha kuharibiwa kwa miundo mbinu kama barabara na madaraja.
Katika Kaunti ya Taita Taveta, watoto wawili walio na miaka mitano na minane ni miongoni mwa watu walipoteza maisha baada ya kuzama majini. Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo, imeendelea kutoa tahadhari ya kutokea kwa mvua na mafuriko zaidi katika maeneo mengi ya nchi hiyo

Comments