Mhe. Biteko awashika mkono WanaIyogelo-Bukombe




 Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko amewachagia mifuko 100 ya saruji kwa lengo la kuwashika mkono wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Shibingo Kata ya Iyogelo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita .
Kabla ya Mhe. Biteko  kuchangia miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi
Biteko aliwapongeza wananchi kwa kuibua miradi ya kujenga shule ya
msingi pamoja na Zanati katika Kijiji hicho cha Shibingo.
Mbunge aliwaomba wanachama wa CCM kuacha tabia ya kuwachukia viongozi
wa vyama vingine vya upinzani huku akiwasisitiza kuwa maendeleo ya serikali ya awamu ya tano hayana chama.
Kwa upande wake Diwani Kata ya Iyogelo Mhe. Juma Lushiku  alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini  Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa kuwachagia wananchi
mifuko 100 ya saruji huku akimhakikishia kuwa atashirikiana na wakazi wa Shibingo na  wananchi wa Kata yake kwa ujumla pamoja na serikali  ili kuhakikisha shughuli za miradi ya maendeleo ziweze kwenda kwa haraka ndani ya Kata hiyo.
Lushiku wakati wa kutoa shukrani hizo alibainisha changamoto za kata yake ilikiwa ni pamoja na miundo mbinu duni ya Barabara,umeme, ukosefu wa Kituo cha Afya na ukosefu wa maeneo ya malisho.

Comments