Afisa
Habari wa Baraza la mitihani la Taifa (Necta), John Nchimbi amesema
mabadiliko hayo katika mfumo wa utungaji wa mtihani wa kuhitimu elimu ya
msingi, aliyatangaza katibu Mkuu wa baraza hilo, Dkt. Charles Msonde
katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika
mjini Dodoma, ambapo sasa kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya
hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yatakuwa ya
kujieleza/kuonyesha njia na jibu ili kupima uelewa wa wanafunzi
watakaofanya mitihani hiyo.
Kwa
maswali 40, kila moja litakuwa na alama 1 na maswali matano kila moja
litakuwa na alama 2 huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye fomu za
OMR na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.
Aidha,
Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa
kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu wasipate shida wakati wa
mtihani huo wa Taifa.
Comments
Post a Comment