Wanachama wa chama cha mapinduzi CCM kupitia jumuiya ya
wazazi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wameipongeza serikali ya wamau ya tano
kwa kupunguza changamoto zinazo ikabili shule ya msingi Namonge kata ya Namonge
tarafa ya Siloka.
Wakati akipongeza jitihada za serikali kwenye maadhisho ya jumuiya wa wazazi kiwilaya
yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Namonge Mjumbe wa Kamati ya
Utekelezaji Jumuia ya Wazazi CCM Mkoa wa Geita John Kafimbi ambaye alikuwa
mgeni rasmi kwenye madhimisho ya wiki ya jumuia ya wazazi CCM kufikisha umri wa
miaka 63 huku akichangia mifuko 10 ya saruji.
Mkuu wa Shule ya msingi Namonge Jemes Kadongo alisema shule
hiyo iliazishwa mwaka 2002 na ina changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa
kutokana na wingi wa wanafunzi kuazia darasa la awali hadi la saba ni wanafunzi
4,000 wasichana 1934 wavulana2066 huku ikikabiliwa na upungufu wa vyumba vyumba 70
kwa sasa vilivyopo 11 mapungufu ya vyumba vya madarasa ni 59.
Kadongo alisema kutokana na upungufu huo serikali imetoa Tsh milion
66.6 kutoka mfuko wa P4R kati ya fedha hizo Sh milioni
60 kwa ajili ya vyumba vitatu vya madarasa Sh 6.6 milioni kwa ajili ya matundu sita ya choo cha
wanafunzi kwa sasa matundu ya choo yanayo tumika 16 wavurana 8 na wasichana 8.
Kadogo aliomba serikali kuendelea kuiangalia shule hiyo
kutokana na kukabiliwa na changamoto nyingine ya upungufu wa walimu mahitaji
walimu 70 waliopo 25 na kwamba upungufu wa madarasa.
Afisa Elimu Shule za Msingi Wilaya ya Bukombe Shadurack
Kabanga alisema fedha hiyo imetoka serikali kuu nakwamba iwapo madarasa hayo
yakikamilikaa ifikapo mwenzi Juni yatasaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi
kubanana darasani.
Kabanga alisema Wilaya ina shule za msingi 78 za serikali na zinakabiliwa
na changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu na madarasa
ingawa wananchi wanaendelea kujenga na serikali inaunga mkono nguvu za wananchi
hao.
Comments
Post a Comment