Wananchi Mkoani Geita wahimizwa kulinda na kutunza
miundombinu ya mabarabara kwa manufaa ya watanzania wote.
Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa barabara ililo jengwa
kwa kiwango cha lami kutoka Uyovu kwenda
Bwanga yenye urefu wa kilomita 45 liligalimu Sh47bilioni mkandarasi amesha
lipwa sh20 bilioni nakuongeza kuwa atakapo fika ikulu atasaini malipo ya
sh27bilioni zilizo baki kwa ajili ya mkandarasi huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli aliwapongeza Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana vizuri na mkandarasi (SINO HYDRO) nakuongeza kuwa Tanzania
anayoiongoza yeye watumishi wa umma wahakikishe wanawasikiliza wanyonge.
Magufuli aliwakumbusha Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri,
Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchini kusimamia agizo lake la kutetea wakulima kwa kutowatoza
ushuru wanapo safirisha mazao yao chini ya tani moja huku akisisitiza wasitozwe
ushuru wa aina yeyote kwani sheria imepitishwa na bunge.
“katika uongozi wangu sitapenda watanzania wa maisha ya chini
wanyanyaswe, nitapenda watanzania waishi kwa amani nitapenda watanzania
washirikiane bila kujali itikadi za dini,ukabila wala vyama vyao watanzania
tudumishe umoja mshikamano na uzalendo na kila mmoja ajipange kuleta maendeleo
ya kuinua uchumi wa nchi yetu”.alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliwahimiza viongozi mbali mbali wa madhehebu
ya dini,wazee,viongozi wa kimila,vijana na kinamama kuombea na kuilinda amani
ya Tanzania ikiwa taifa limekaa kwa amani zaidi ya miaka 50 na kuwa mfano kwa
mataifa mengine
Aliwaomba wakulima na wafungaji kuwa wavumilivu wakati
serikali inajipanga kukata sehemu ya maeneo ya mapori ya hifadhi za serikali kuwa ardhi ya makazi na eneo la kufanyia
shughuli mbalimbali za kibinadamu huku akiwaahadi wakulima na wafugaji kuwa
atalisimamia na kuhakikisha wanafaidika na jasho lao lengo ni kuimarisha maisha
ya watanzania ki uchumi.
Aliwapongeza watumishi wa Tanroads akiwemo Mhandisi Mfugale kwa
kufanya kazi nzuri pamoja na wenyeviti wa bodi na kuwasihi waendelee kusimamia
barabara, “nawakumbuka sana natamani kurudi kwenye Wizara ya Ujenzi kwasababu
ni Wizara nimeka katika maisha yangu miaka 17 watumikieni watanzania”.Alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliwaomba wananchi kuto badilika badilika
katika uchanguzi kwani mwaka 2015 walichaguwa Mbunge mzuri na kwamba amekuwa
mwenyekiti wa kamati ya madini amefanya vizuri akaenda kuchunguza madini ya
tanzanite amefanya vizuri na hatimae kumuona kumteuwa kuwa Naibu Waziri wa Madini
na anafanyakazi nzuri mpeni ushirikiano.
Awali Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Elias Kwandikwa
akimkalibisha Rais Magufuli kuongea na mamia ya wananchi waliohudhulia kwenye
viwaja vya eneo la kanisa katoriki Kata
ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita waliotoka vijiji mbali mbali vinazounda
Wilaya ya Bukombe kwa ajili ya kumsikiliza.
Kwandikwa alisema
barabara ya Uyovu kwenda Bwanga yenye urefu wa kilomita 45 inaunganisha barabara
ya Busagara,Geita, na Bihalamulo, yenye urefu wa kilomita 220.
Alisema pia barabara ya Uyovu Bwanga inaunganisha barabara
kuu ya kutoka Isaka Ushirombo Lusumo yenye kilomita 374 barabara hii
imeunganisha wananchi wa Mkoa wa Geita Shinyanga Kagera Kigoma na nchi jirani
za Burundi, Rwanda na nchi ya kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) na Uganda.
Kwandikwa alibainisha malengo ya utekelezaji wa mradi huu ni
kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo kuazia wakulima na wavuvi wafanya biashara
wanakuwa na barabara zinazo pitika munda wote, kukamilika kwa mradi huu
kumefungua furusa ya kusafirisha watu na bidhaa.
Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Bukombe Mbunge wa Jimbo la
Bukombe pia Naibu Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko alimshukuru Rais
Magufuli kwa kufika tena kuonana na wananchi wa Wilaya ya Bukombe wananchi waliokuwa
wamemkumbuka na ahaidi zake alizozitoa kwenye kampeni vitendo vyake vimedhibitika
kwa vitendo.
“kunamiradi ilikuwa haipo lakini umetumwagia fedha ikiwemo
kumaliza changamoto ya shule ya msingi Ibamba uliitatua kero hiyo ,pia umetoa Sh500
milioni kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa chumba cha upasuaji kituo cha afya
Ushirombo na kituo cha afya Uyovu Sh 400 milioni kwa ajili ya ujenzi wa wondi
ya mama na mtoto pia magari mawili ya kubeba
wagonjwa kituo cha afya Uyovu na kituo cha afya Ushirombo Rais anajuwa shida za
watanzania wananchi wanasema ni mwambie zile kilomita tano za lami anajuwa
barabara ya ushirombo katoro kuwa wananchi wanaomba liwekewe lami anajua maji
kutoka ziwa viktoria amesha tenga Sh1,7 Bilioni anajuwa munahitaji maji kutoka
ziwa viktoria mimi siwezi kusema na wanaotaka nimwambie Rais kilakitu anajuwa”alisema
Biteko.
Biteko aliwaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono na
kumuombea Rais Magufuli aendele kutetea haki za wa watanzania wa maisha ya
chini na kuleta mabadiliko ya taifa hasa katika kupandisha uchumi wa taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Luhumbi kwa niaba ya wananchi wa
Mkoa wa Geita alimshukuru sana Rais Magufuli kuja kufungua barabara hiyo ambayo
inachochea maendeleo ya kiuchumi na fursa
za kiuchumi na kijamii kwa kiasi kikubwa ikiwemo na ukuwaji wa sekta za kibiashara
sekta ya kilimo na kurahisisha usafirishaji watu na mazao barabara hiyo
itachochea ukuaji wa sekta ya utalii na kuongeza pato la Mkoa na taifa kwa
ujumla.
Mkazi wa Kata ya Uyovu Letisia Mourice alisema serikali
imefanya vizuri kutengeneza barabara hiyo kwani kumewaondolea changamoto ya
kusafiri kwenda Bwanga walikuwa wana tumia masaa mawili barabara lilikuwa bovu
lakini kwa sasa watasafiri kwa magari watatumia dakika 40 hali ambayo
itawafanya kuwa na mzunguko mkubwa wa kiuchumi na kurahisisha ndugu na jamaa kufika
kwenye huduma za afya mapema.
Comments
Post a Comment