Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Kampuni ya OreCorp Tanzania Limited (hawapo pichani) walipokutana kwenye Ofisi za Afisa Madini Mkoa wa Geita. |
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mbele katikati) akizungumza na wawakilishi wa Kampuni ya Ore Corp Tanzania Ltd. |
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko amezikumbusha Kampuni za Madini nchini
kuhakikisha suala la mahusiano na jamii linapewa kipaumbele ili
kuboresha utendaji wa shughuli zao.
Amesema
hayo Machi 5, 2018 Mkoani Geita alipokutana na wawakilishi wa Kampuni
ya OreCorp Tanzania Limited yenye Leseni ya Utafiti ambayo inatarajia
kuanzisha shughuli za uchimbaji mkubwa wa dhahabu kwenye eneo la
Nyanzaga, Wilayani Sengerema.
Katika
mkutano huo uliofanyikia kwenye Ofisi za Madini, masuala mbalimbali ya
shughuli za uchimbaji madini yalijadiliwa na msisitizo ukiwa kuhakikisha
suala la uboreshaji wa mahusiano na jamii zinazozunguka miradi linapewa
kipaumbele.
Biteko
alisema uboreshaji wa mahusiano na jamii ni kwa faida ya kampuni kwani
kufanya hivyo kutasaidia kuepuka migogoro isiyo ya lazima na hivyo
kuboresha utendaji kazi na kuwa na uzalishaji wenye tija.
Aidha,
awali kabla ya kukutana na kampuni hiyo, Biteko alikutana na Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahya
Samamba na Afisa Madini Mkoa wa Geita, Mhandisi Ally Maganga.
Comments
Post a Comment