Aliyekuwa Rais Wa Ufaransa ahojiwa Kuhusu Fedha za Gaddafi.


Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameripoti hii leo katika kituo kimoja cha polisi nchini humo, ambako alitarajiwa kuhojiwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi juu ya tuhuma zinazohusiana na fedha zilizotumika kufadhili kampeni yake wakati wa uchaguzi. Gazeti la Le Monde limemnukuu afisa mmoja wa mahakama nchini Ufaransa akisema kuwa uchunguzi huo unahusisha tuhuma kuwa utawala wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, ulifadhili kampeni za Sarkozy katika uchaguzi wa mwaka 2007. Hata hivyo, mwanasheria wa Sarkozy hakupatikana mara moja kwa ajili ya ufafanuzi zaidi.

Comments