Hawa ni baadhi tu ya wanafunzi wa kitengo cha elimu maalum kilichopo Shule ya msingi Ushirombo.
Vyumba vya Madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kitengo cha elimu maalum
Katibu wa Wazazi Mkoa wa Geita Joseph Mwita akizungumza na wanaccm katika maadhimisho yaliyofanywa na Jumuiya ya Wazazi Ccm(W)Bukombe katika shule ya Msingi Ushirombo kitengo cha elimu maalum.
Meza Kuu
Wajumbe.
Mmoja ya Wajumbe akizungumza katika hafla hiyo.
Katibu wa Wazazi Mkoa wa Geita Joseph Mwita akiendesha zoezi la upandaji miti katika shule hiyo
Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamefanya
maadhimisho ya miaka 41 ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuwatembelea
wanafunzi wa shule ya msingi Ushirombo kitengo cha elimu maalum na kufanya
usafi,changizo la kiasi cha shilingi elfu themanini na kushiriki nao
kwenye chakula cha mchana shuleni hapo.
Katika maadhimisho hayo Katibu wa wazazi Mkoa wa Geita Joseph Mwita amewashukuru
wanachama kwa uamuzi wao wa busara
kwenda kuwaona watoto hao huku akisisitiza zoezi hilo kutokukomea leo.
Pia waalimu wa shule hiyo walibainisha changamoto zao ikiwa ni ukosefu wa usafiri kwa
watoto kwani asilimia kubwa ya watoto hao hawajiwezi kwenda na kutoka shuleni peke
yao,upungufu wa miundo mbinu ya madarasa kulingana na ongezeko la idadi ya wanafunzi hao
kwa sasa pamoja na vifaa vya michezo.
Aidha Katibu wa wazazi Mkoa wa Geita Joseph Mwita amewaomba wanachama
wa CCM na wananchi kwa ujumla wajitahidi kuwahudumia watoto hao sambamba na
kuwafichua kwa pamoja baadhi ya watoto wenye ulemavu waliofichwa na wazazi wao au walezi majumbani bila
kupata elimu ili nao waweze kujipatia elimu.
Comments
Post a Comment