Meza Kuu
Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Wilaya ya Bukombe Leticia Mourice akisoma risala
Mhe. Diwani wa Kata ya Igulwa akila keki
Wamama wanaowekeza pesa zao katika jukwaa la wanawake Wilayani Bukombe wametakiwa kuzitumia fedha wanazozipokea kutoka kundi hilo ili kujiimarisha kimaisha.
Akizungumza katika sherehe iliyojumisha vikundi kumi na sita vya Kata ya Uyovu walipokutana kwa ajili ya kugawana faida,kufahamiana na kubadilishana uzoefu.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko wakati akijibu changamoto za wamama hao alianza kwa kuwapa taslimu milioni moja kwa ajili ya kuinuia mfuko wa umoja wa wanawake hao sambamba na kuwasisitiza kutafuta eneo la kujenga ofisi kwa ajili ya kuongeza thamani ya umoja huo na kupata sehemu ya kudumu kwa ajili ya ujasiliamali hali iwatakayowapa jumuiya zingine kuona mfano ndani ya Kata ya Uyovu na Wilaya nzima ili kupunguza wimbi la wasio na ajira huku wakimuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika Tanzani ya Viwanda
Comments
Post a Comment