NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. DOTO MASHAKA BITEKO AANZIA MKOA WA GEITA


 Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita pamoja na wataalam wa Madini wa Mkoa huo alipofanya ziara yake ya kwanza baada ya kuapishwa ikiwa ni hatua madhubuti ya kutekeleza majukumu yake
  Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb)akisaini katika Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kuwasili Wilayani Bukombe
Wajumbe wa Kamati ya Siasa na wanaCCM Wilayani Bukombe wakimpokea Naibu Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko alipowasili katika Ofisi hiyo ya Chama cha Mapinduzi-Bukombe
Mwenyekiti wa CCM(W)Bukombe Daniel Machongo akizungumza katika ugeni wa Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko baada ya kuwasili Wilayani hapo ikiwa ni ziara ya kikazi


Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa katika Mgodi unaomilikiwa na Stephan Spimo alipokwenda kwa ajili ya kujionea hali halisi ya mgodi huo.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na wataalamu wa Madini Mkoa wa Geita pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bukombe walikijionea shimo lililoleta maafa ya Bwn Mvumbi Msuluzya baada ya kufunikwa na kifusi hadi mauti.


 


 

 
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akitoa rambirambi kwa Mjane(mke wa marehemu bwn Mvumbi Msuluzya) aliyefunikwa na kifusi hadi mauti.

Comments