Wazazi na walezi ambao hawajawapeleka wanafunzi
waliofaulu kuanza kidato cha kwanza kuanza kusakwa wakiwemo wanafunzi wenyewe.
Agizo hilo la kuazishwa msako lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi
Robert Luhumbi wakati akipokea taarifa ya uadikishaji wa wanafunzi kitado cha
kwanza mwaka 2018 iliotolewa na Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bukombe wakati wa ziara
yake ya kikazi Wilayani Bukombe.
Luhumbi aliagiza msako huo kuanzia Januari 22 kuwasaka
wanafunzi na kuwakamata wazazi na walezi ambao hawaja wapeleka wanafunzi
kuadikishwa na kuhakikisha wanafunzi
wote wanapelekwa shule.
Awali Afisa Elimu shule za Sekondari Wilaya Philibert Nyangahondi alisema Wilaya ina shule
14 za sekondari za serikali ambapo
zilitakiwa kupokea jumla ya wanafunzi 3985.
Nyangahondi alisema wanafunzi wa kitado cha kwanza
wanaotakiwa kuripoti ni 3985 hadi kufika
Ijumaa ya januari 19 mwaka huu walikuwa wamelipoti wanafunzi 2829 bado
wanafunzi 1156 ambao haijulikani walipo.
Mkuu wa Mkoa Mhandisi Luhumbi aliagiza kamati za ulinzi na
usalama Wilaya zote za Mkoa wa Geita
kuwashukia viongozi ngazi ya Kijiji ili kuhakikisha wanafunzi wanaripoti
shuleni na waliofikia umri wa kuadikishwa darasa la kwanza wanapelekwa shule.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga alimhakikishia Mkuu wa Mkoa atatekeleza agizo hilo mapema.
Maganga aliwaomba wazazi na walezi kupeleka wanafunzi mashuleni
kabla ya kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Comments
Post a Comment