Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amepiga
marufuku bodi na kamati za maendeleo ya shule kuratibu michango kwa wazazi na
walezi mashuleni.
Luhumbi aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya fedha Sh
milioni 60 toka P4R ambazo zimeelekezwa na serikali kujenga
vyumba vya madarasa sita katika shule ya
sekondari Ushirombo huku bodi ya shule hiyo ilikuwa inakusanya tofari tatu toka
kwa wazazi kwa ajili ya ujezi huo.
Luhumbi alibaini kuwa ripoti
aliyoipokea ilikuwa na nia nzuri lakini imefanyika katika mazingira mabaya
kunamahitaji ya vyumba vya madarasa
lakini bodi ya shule hiyo iliwataka wazazi na walezi kukubaliana
kuazisha ujenzi kwa michango ya tofari
tatu hali ambayo inaathiri taratibu zinazotaka kutowaumiza wazazi kwani
miongoni mwao kunawananchi wanaishi mazingira magumu wakiwemo wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii
TASAF.
Alisema serikali
haitaki kuweka michango kwa mzazi yeyote badala yake michango ya kuchangia
maendelo ya ujenzi wa shule zahanati wahusishwe wananchi wote na sio
wazazi shuleni, wanafunzi wasirudishwe
nyumbani kwa tatizo la michango alisema Mkuu wa Mkoa Luhumbi.
Luhumbi alisema kutokana na hii taarifa kunakundi kubwa
liliachwa kushirikishwa wakiwemo wadau wa Elimu na wafanyabiashara huku
akiwasihi madiwani kufanya mikutano ya hadhara kuhamasisha michango ya hiyali
kwenye miradi ya maendeleo.
Akiwa shuleni hapo Mkuu wa Mkoa Luhumbi, wananchi walimunga
mkono na kufanya harambee fupi na kufanikisha kukusanya mifuko 84 ya saruji
fedha Sh 110,000 tofari 30 za sementi na tripu za mchanga 2 kutoka kwa
wananchi.
Luhumbi aliwata wahusika wa mradi wa ujenzi wa madara sita na
ofisi mbili za walimu hadi kukamilia zisitumie Sh 60 milioni nakuwashauri kutoa tenda za ujenzi kuanzia kuchimba msingi
na kazi ndogo ndogo washirikishwe wananchi ili kuokoa gharama zisizo kuwa za
lazima ili kuokowa fedha hizo ili zitakapo baki zifanye kazi nyingine ya
maendelo .
Awali mkuu wa shule ya Ushirombo Sekondari Juma Luguhwa
alisema kikao cha desema 14 cha wazazi
kilichotanguliwa na kikao cha walimu cha Desemba 7 kikifatiwa na kikao cha Bodi cha Desemba 15 wazazi na walezi
walikubaliana kuazisha ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili kila mwanafunzi anaesoma hapo mzazi alete
tofari tatu.]
Luguhwa alisema walitarajia kukusanya tofari 4,545 hadi Rais
Dk John Magufuli anazuia michango walikuwa wamekusanya tofari 1,038 na kwamba Desemba 29 mwaka 2017 shule
iliigiziwa fedha Sh 60 milioni kutoka mfuko wa P4R kikao kilihudhuliwa na
wazazi 100 lakini wako zaidi ya 200.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo
amempongeza Mkuu wa Mkoa kufika kuwaunganisha viongozi na wananchi na kuwapa
Elimu ya kuto chagishwa shuleni badala yake wachangie kupitia mikutano ya
serikali itakayofanywa na madiwani kuhamasisha michango ya hiyali ya maendeleo
kwa wananchi ili kukamilisha miradi.
Comments
Post a Comment