MHE. DOTO BITEKO AVUNA WANACHAMA WAPYA KUTOKA CHADEMA KATIKA TAWI LA KIZIBA


Mapokezi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM wakielekea maeneo ya Ofisi yao ya Tawi la kiziba kwa ajili ya uwekajiwa jiwe la msingi
mwonekano uliyofikiwa na wana CCM katika hatua ya ujenzi
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akikata utepe kwa ajili ya uwekaji wa Jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM Tawi la Kiziba Kata ya Ushirombo Wilayani Bukombe.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko,Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lameck Warangi na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa wakijadiliana nini mstakabali wa kuhakikisha wana malizia ujenzi wa madarasa ya Shule hiyo ya msingi Kiziba  baada ya Mbunge huyo kutoa mifuko arobaini ya saruji ikiwa ni hatua ya kuhakikisha vyumba hivyo vinaisha na kupunguza kama sio kumaliza changamoto za ukosefu wa madarasa shuleni hapo.
Baadhi tu ya vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Kiziba
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akipewa heshima ya ufalme na wamama wa CCM-Kiziba

Mmoja ya kikundi kilichotumbiza katika kusanyiko hilo
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiungana na watoa burudani




Wanachama Wapya waliovunwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kutoka Chadema na kuhamia Chama Cha Mapinduzi
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wakazi wa Kiziba baada ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Ofisi yao ya Tawi sambamba na kutoa tofali elfu saba za kuchoma kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo.

Comments