UZINDUZI WA MRADI WA UMEME REA AWAMU YA TATU KUFANYIKA WILAYANI BUKOMBE

 Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Medard Kalemani akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu Wilaya ya Bukombe
  Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Medard Kalemani akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

  Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Medard Kalemani akisalimiana na wajumbe wa Kamati ya Siasa katika Ofisi ya CCM (W)Bukombe.
 Mwenyekiti wa CCM(W)Bukombe ndg. Daniel Machongo
 Meza kuu wakiwa Mkutanoni katika kijiji cha Bulega
  Waziri wa Nishati Mhe.Dkt  Medard Kalemani akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CCM(W)Bukombe Daniel Machongo,  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiteta jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Wilaya Bukombe Ladislaus Soku
 Diwani wa Kata ya Bulega Mhe. Eric Kagoma akizungumza na wananchi wa Kata yake
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Safari Nikas Mayala akisema na hadhara ya wakazi wa Bulega
 Wakazi wa Bulega wakiwa Mkutanoni
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwasisitiza wakazi wa Bulega juu ya kufanya shunguli za maendeleo.
 Mkuu wa Wilaya Bukombe Josephat Maganga akizungumza na wakazi wa Bulega
  Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Medard Kalemani akizungumza na wakazi wa Bulega alipokwenda kwa ajili ya uzinduzi wa utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini REA Wilayani Bukombe

Wasimaminzi wa Mradi wa REA Wilaya ya Bukombe  toka Kampuni ya (WHITE CITY GUANDONG JV LTD )

  Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Medard Kalemani akiwa amebeba kifaa kiitwacho Umeme Tayari(UMETA) na kukielezea umuhimu wake kwa wananchi wa kipato cha chini
  Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Medard Kalemani akimkabidhi kifaa hicho cha UMETA mmoja wa wananchi wasiojiweza.


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Wilaya ya Bukombe. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 30/12/2017 katika kijiji cha Bulega, Kata ya Bulega, Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita alikuwa ni  Waziri wa Nishati  Dk. Medard Kalemani.

 

Katika uzinduzi huo Dk Kalemani alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko kwa kazi anazo zifanya za kuleta maendeleo jimboni kwake na taifa kwa ujumla.


Alisema Biteko amekuwa akimsumbua mara kwa mara akiiomba serikali impe umeme  kwa niamba  ya wananchi kwa upendeleo serikali ikatekeleza mradi wa umeme vijiji REA awamu ya tatu Wilaya ya Bukombe ukilinganisha na sehemu zingine  ikiwa 
vitongoji vyote 70  ndani ya vijiji 52 Kata 17 Tarafa tatu zinazo unda Wilaya ya Bukombe wananchi watanufaika na umeme wa REA.



Dk Kalemani aliwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Bukombe januari 15 mradi utakuwa umekamilika na Januari 20 vitongoji 70 wananchi watawashiwa umeme na kwamba mkandarasi atakaye chelewesha mradi huo bila sababu za msingi na kubainika hayupo kwenye eneo la kazi atachukuliwa hatua na kuongeza kuwa  watakaopewa kipaumbele ni wananchi  wa eneo husika kwa kupewa ajira ndogo ndogo kama uchimbaji wa mashimo na ubebaji wa nguzo na kusisitiza kuwa wananchi hakuna atakae lipwa fidia .

Awali Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga wakati akimkaribisha Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani alisema kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya 2012 wilaya inawatu 224,542.


Maganga alisema kiwango cha ongezeko la watu ni asilimia 5.9 Wilaya imezungukwa na hifadhi asilimia 72 asilimia 28 nimaeneo ya makazi na biashara kwa sasa Wilaya inakadiliwa kuwa na watu 258,405 ongezeko linachangiwa nawatu kuzaliana.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara Kata ya Bulega aliwaomba wananchi  kuchagamukia frusa za kupata umeme wa REA kwa kuazisha biashara zinazohitaji umeme hali ambayo itawainua kiuchumi na kuongeza pato la familia.
Biteko aliishukuru serikali ya awamu ya tano na Waziri wa Nishati Dk Kalemani ambae ni Waziri wa kusema na kutenda  kwa kupokea ombi la mahitaji ya Wananchi wa Bukombe kati ya  vitongoji  70 ndani ya vijiji vinavyo unda tarafa tatu vya Wilaya ya Bukombe
wananchi watapata Umeme wa REA  hali ambayo itawafanya wananchi kufanya kazi za kujikwamua katka wimbi la umasikini.



.

Comments