NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ABDALLAH ULEGA AKERWA NA UUZWAJI WA MIFUGO KIHOLELA

 Ng'ombe waliotafishwa wakiwa kwenye zizi lao kabla ya mnada kuanza 
Hili ni moja ya kundi la Ng'ombe wakiwa tayari eneo la mnada
Mnunuzi akiwatoa ng'ombe eneo la mnada baada ya kufanya malipo
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wafugaji wa Wilaya ya Bukombe katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
 
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa Wilaya ya Bukombe katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
 Wafugaji wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega. 
Hawa ni baadhi tu wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Bukombe.

 

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita  katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la juni 15 mwaka 2017 alipokuwa na wataalamu wa idara ya mifungo Dodoma  na kuzitaka halmashauri  zote nchini kuweka chapa kwenye ng’ombe.
  Wilaya ya Bukombe imetekeleza kwenye Kata 13 kati ya Kata 17 tangu Oktoba 3 mwaka 2017 huku Wilaya ikiwa na jumla ya ng’ombe 130,750 na waliopigwa chapa wakiwa ng’ombe 95,743 sawa na asilimia 73. 
Kauli hiyo alitolewa na Katibu Kawala wa Wilaya ya Bukombe Paul Cheyo wakati  akitowa taarifa kwa Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akiwa Wilayani hapa kwa ajili ya kuwapa pole wafugaji kwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya askari wa wanyama pori  wasio waadilifu kwa kufanya kitendo cha kukamata mifugo ya wafugaji na kuiuza kabla ya kufungua mashitaka mahakamani.
 Alisema Wilaya ya Bukombe inaeneo dogo la makazi huku kukiwa hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo
.
Cheyo alisema Wilaya inakabiliwa na upugufu wa maeneo ya marisho hakuna maeneo yaliyotegwa  hali ambayo inapelekea kuwa na mgogoro mkubwa kati ya wafugaji na askari wa wanyama pori katika pori la hakiba la Kigosi Muyowosi 
.
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wilaya ya Bukombe  (CHAWAKAZI) Petero  Kazala alisema kwa sasa ni masikini kwani ng’ombe wake 170  walikamatwa na askari wa wanyamapori  Novemba 16 wakitoka malishoni ndani ya pori hilo wamepigwa mnada Desemba 21 bila kushirikishwa ingawa alikuwa anawafata ili alipe faini, alipewa majibu kuwa asubiri kuitwa mahakamani hatimae mifugo kuuzwa bila mhusika kuitwa mahakamani hata siku moja aliyasema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri wa Mifungo na uvuvi kuwa pengine kuna wafugaji wanapokamatiwa ng’ombe zao wanazikimbia.

Kazala alisema hukumu ilitolewa na Mahakama ya Wilaya Novemba 5 mwaka huu wafugaji wengi wamefirisika na kurudia hali ya umasikini kutokana na kamata kamata hii na wamekuwa hawashirikishwi  wafugaji wakati wa munada aliongeza kuwa ng’ombe wanauzwa kabla ya siku ya munada.  

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko alisema haitatokea  mwananchi jamii ya wafugaji kupewa pori la akiba kwa ajili ya marisho  ya ng’ombe badala yake kuna mapendekezo ya sheria itakapo badilishwa  na Bunge Februari 2018 badala ya adhabu ya kumfilisi mfungaji atozwe faini
watu wa maliasili hawapaswi kulaumiwa bali nina laani kitendo kinacho fanywa na baadhi ya watumishi wa umma idara ya maliasili kwa nia mbovu ya utekelezaji wa sheria   iliyoko nyuma ya sheria alisema Mhe. Biteko.

Mhe. Biteko aliongoza kwa kusema askari wa wanyamapori wamekuwa wanauza ng’ombe kabla ya munada, huku  wamiliki wapo na hawaja pelekwa mahakamani,wamekuwa na maamzi ya kuuza kwa makusudi hatakama kuna amri ya mahakama ng’ombe zisiuzwe,  aliongeza kuwa ushahidi  upo kuna oda ya mahakama kuu ya rufaa ilizuia kuuzwa ngo’mbe 603 wilayani hapa lakini waliuzwa kwa nguvu kwa kutekeleza hukumu iliyotolewa na mahaka ya wilaya ya Bukombe.
Mbunge aliwaomba wafugaji kuacha tabia ya kuzungukana imekuwepo tabia miongoni mwao wafugaji kuwafanyia biashara wafugaji wenzao kwa kushirikiana na watumishi wa umma idara ya maliasili wanaolinda pori la akiba la kigosi Muyowosi .

Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi  Mhe. Abdallah Ulega alisema kuwa wafugaji wawe wavumilivu wakati Bunge linaenda kubadilisha baadhi ya sheria za wanyamapori  kama alivyosema Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) na kwamba kuna watumishi wa umma wamekuwa wakitekeleza majukumu kwa kuvunja sheria za mifungo ukweli ni kwamba hifadhi ni ya muhimu mifungo nayo ni ya muhimu pia ndio maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe Dkt John Pombe Magufuli akaiweka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya kushugulikia kero na changamoto za wafugaji.

Ulega alisema kwa kweli kitendo cha minada ya mifungo inayoendelea kufanyika ki holela Wilayani Bukombe imenikera sana naomba minada hiyo isiwe mingi badala yake zitumike hekima na busara ili kuwajengea imani wananchi na serikali yao wasione kama imewatenga wafugaji 

Naibu Waziri aliomba Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya kuhakikisha inafatili watumishi wa umma wanao jihusisha na ukiukaji wa maadili kwa kuwanyanyasa wafugaji na kiusisitiza halimashauri kukamilisha agizo la waziri mkuu kuweka chapa kila ngo’ombe ili ng’ombe za watanzania ziweze kujulikana.

Comments