MHE. DOTO BITEKO AJITOA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA ELIMU


 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe . Doto Mashaka Biteko akimwelekeza Katibu wake bwn Benjamini Mgeta sehemu zinazohitajika marekebisho ikiwa ni hatua ya kuhakikisha vyumba hivyo vinaanza kufanya kazi ifikapo januari baada ya kuamua kwa dhati kutoa fedha zake kwa ajili ya umaliziaji wa Shule hiyo ya Msingi Lyobahika baada ya kujengwa kwa nguvu za wananchi na hatimae kusimama tangu mwaka 2009.
 Katibu wa Mbunge Bwn Benjamini Mgeta.
 Katibu wa Mbunge Bwn Benjamini Mgeta akimwonyesha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko maeneo ya Shule ya msingi Lyobahika na mipaka yake.

 Choo Cha Shule hiyo ya msingi Lyobahika.
  Choo Cha Shule hiyo ya msingi Lyobahika baada ya umaliziaji
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akitazama hatua iliyofikiwa katika umaliziaji wa vyumba vya madarasa katika Shule ya msingi Kanembwa baada ya kunyoosha mkono wake pia ikiwa ni hatua ya kuboresha miundo mbinu ya elimu katika Jimbo la Bukombe.


 Hili ni darasa lililojengwa zamani Katika shule ya msingi Kanembwa na kwa sasa liko katika hali hatarishi ya kuwaponda wanafunzi wanaopata elimu kupita darasa hilo hali iliyosababisha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kuamua kujitoa fedha zake binafsi  kwa ajili ya kukinusuru kizazi kinachosomea kwenye darasa hilo
Hii ni picha ya zamani ya mwonekano wa Jengo la vyumba vya madarasa shule ya msingi Kanembwa vilivyokuwa vimesimama kwamda mrefu  kabla Mhe. Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko  kuweka mkono wake.



 Mwonekano wa Vyumba vya Madarasa ya Shule ya Msingi Kanembwa baada ya Mkono wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.

Comments