KAMATI YA USHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE NA MBOGWE ZAKUTANA KUFANYA MGAWANYO WA RASILIMALI NA MADENI

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Ndg Josephat Maganga akizungumza kwenye kikao cha kupitia mapendekezo ya mgawanyo wa Rasilimali na Madeni kati ya Halmashauri (Mama) ya Wilaya ya Bukombe na Halmashauri mpya ya Wilaya ya Mbogwe kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Ndg. Martha Nkupasi akisisitiza jambo katika kikao hicho. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Bukombe Ndg Daniel Machongo na  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Mbogwe Mama Johari kwa pamoja wakiwa katika umakini wa kufuatilia mwenendo mzima wa kikao hicho.
 
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bi. Sara Yona akisoma taarifa za Rasilimali na Madeni kati ya Halmashauri (Mama) ya Wilaya ya Bukombe na Halmashauri mpya ya Wilaya ya Mbogwe.

Wakuu wa Idara mbalimbali kutoka Halmashauli ya Wilaya ya Mbogwe wakisikiliza ajenda kwa umakini.

Hawa ni baadhi tu ya watendaji wa Kata mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Wakuu wa idara mbalimbali wakiwa mchanganyiko na watumishi wengine kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe katika umakini mkubwa kabisa ndani kikao hicho.
Wajumbe wakiwa ukumbini.

Comments