DOTO BITEKO; NAMONGE ENDELEENI KUIBUA MIRADI YA MAENDELEO NIKO NYUMA YENU


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya Kata ya Namonge pamoja na baadhi ya wataalam wa Kata hiyo wakitazama hatua iliyofikiwa katika umaliziaji wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Ilyamchele.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya Kata ya Namonge pamoja na baadhi ya wataalam wa Kata hiyo wakitazama ujenzi wa Choo cha Shule ya msingi Ilyamchele.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya Kata ya Namonge pamoja na baadhi ya wataalam wa Kata hiyo wakielekea eneo la mkutano kwa ajili ya kuzungumza na wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya Kata ya Namonge pamoja na baadhi ya wataalam wa Kata hiyo wakitazama msingi wa zahanati ya Ilyamchele iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na wakazi ya Kijiji cha Ilyamchele.
Diwani wa Kata ya Namonge Mhe Mlalu Bundala akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ilyamchele
Kikundi kilichotumbuiza kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko katika Kijiji cha Ilyamchele.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wakazi wa Ilyamchele






Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko akimkabidhi  fedha bibi wa mtoto kwa ajili ya huduma za mtoto mlemavu



 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita,Mhe Doto Mashaka Biteko amewachagia mifuko 58 ya saruji kwa lengo la kuwashika mkono wananchi waliotumia nguvu zao katika ujenzi wa shule ya msingi Ilyamchele na mifuko mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Namarandula katika Kata ya Namonge .

Kabla ya Mbunge kuchangi mradi wa maendeleo ulioibuliwa na wananchi Biteko aliwashukuru kwa kumchangua siku ya uchaguzi Oktoba 25 mwaka 2015 na kwamba hawezi kumripa mtu mmoja mmoja, kazi yake atahakikisha anawatumikia na kutetea wananchi wa Bukombe ili wapate maendeleo.

Biteko wakati alipozungumza nao kwa nyakati tofauti aliwapongeza wananchi wa Ilyamchele na Namarandula kwa kuibua mradi wa kujenga shule ya msingi na Zahanati huku akiwasisitiza wananchi kuzidi kufanya kazi kwa pamoja bila kujali tikadi zao kwani maendeleo hayana dini wala chama.

Pia aliwahakikishia wananchi wa Kata hiyo ya Namonge kupunguza kama sio kumaliza kabisa changamoto za umeme na uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara ifikapo 2018 sambamba na kuhakikisha shule ya msingi Ilyamchele inasajiliwa na kutambulika kisheria. 

Upande wa  wananchi walibainisha changamoto zao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya maji safi,manyanyaso ya askari wa maliasili, usajili wa shule ya msingi Ilyamchele hali itakayo waepushia wanafunzi hao kwenda shule nyingine kwa ajili ya kufuata kituo cha mtihani,kuchelewa kufumguliwa kwa soko lao la kisasa la udaga huku changamoto kubwa ikiwa ni ukosefu wa miundo mbinu ya barabara ndani ya Kata hiyo.
 



Comments