Vikosi vya Basketball vikiwa uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017
Vikosi vya Mbio za baiskeli vikiwa uwanjani katika ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017
Vikosi vya Volleyball vikiwa uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017
Vijana wa Karate wakiwa uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017
Vijana shupavu wakionyesha uwezo wao uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017Vikosi mbalimbali vikiwa pamoja na mashabiki tayari kwa maandamano ya pamoja na kupokea ujumbe wa Bonanza la Doto Cup 2017
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akitoa ujumbe wa Bonanza la Fainali ya Doto Cup 2017 mara baada ya kuwasili mgeni rasmi.
Vikosi vya wakimbia kwenye magunia wamama vikiwa uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Fainali Doto Cup 2017
Mshindi wa kukimbiza kuku upande wa wanaume
Mshindi wa kukimbiza kuku upande wa wanawake
Mashabiki na wanachama wa Simba na Yanga wanaume wakipimana nguvu uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Said Kiganja akikagua wachezaji wa Netball ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Said Kiganja,Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb),Mwenyekiti wa CCM(W) Daniel Machongo na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe wakiwa na wachezaji wa Timu ya Runzewe Academy Fc katika Picha ya Pamoja kabla ya mchezo kuanza wa Fainali ili kumpata mshindi wa Ligi ya Doto Cup 2017.Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Said Kiganja,Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb),Mwenyekiti wa CCM(W) Daniel Machongo na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga wakiwa na wachezaji wa Timu ya Chui Fc kutoka Bugerenga katika Picha ya Pamoja kabla ya mchezo kuanza wa Fainali ili kumpata mshindi wa Ligi ya Doto Cup 2017.
Wana-Bukombe wakishuhudia uhondo wa michezo mbalimbali katika Bonaza la Fainali hiyo ya Doto Cup 2017.
Timu
ya Runzewe Academy Fc imetwaa ubingwa wa lingi ya Doto Cup 2017 kwa kuichapa timu ya Chui fc iliyoko
Bugelenga gori 8 -7.
Wafungaji
wa magori ya Runzewe Academy John Ngasa dakika ya 18 kipindi cha kwanza na
Leonard Figo dakika ya 80 kipindi cha pili huku magori 6 yakifungwa kwa mikwaju
huku gori la ushindi lilifungwa na Rashid Sanga kwa penaliti.
Magori
ya Chui fc yalifungwa na Jonas Jemes dakika ya 50 na Musa Jemes dakika ya 66 na
wakati wa kucheza matuta kutokana na dakika 90 kuisha bila kupatikana mshindi
wa chezaji wa Chui fc walifunga magori kwa penaliti 5 na kuchukuwa nafasi ya
pili.
Mbunge
wa jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko mudhamini wa lingi hiyo alisema
lengo la kuandaa mashindano nikuwatambua
na kuwainua vijana kimichezo.
Mhe.
Biteko wakati akimuomba Katibu Mtendaji
Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania kuvionea kipaumbele vipaji vya vijana wanao
ishi kwa kucheza ndodo ili wakapatiwa na fasi kwenye timu kubwa za taifa.
Katibu
msaidizi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Bukombe (BUFA) Erasto Banunu
alisema ligi hiyo iliaza Julai 15 mwaka huu na kushirikisha vilabu 128 michezo
waliyo cheza hadi siku ya fainali michezo 120.
Alisema
wilaya ya Bukombe inavijana wenye vipaji kwenye Soka lakini hawana wakuwaendeleza
hivyo kupitia Baraza la Michezo na TFF ilete walimu wakufundisha na kutambua
vipaji kwa vijana.
Katibu
mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Said Kiganja ambae alikuwa mgeni rasmi
kwenye fainali ya Doto Cup 2017 kabla hajakabizi zawadi alimpongeza Mhe Mbunge
kwa kuisaidia serikali kujibu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ibara
ya 161.
Kiganja
alikubali ombi la Mbunge na kumtaka kufanya mambo ya fuatayo mwaka 2018 atakapo
kuwa anafanya madalizi ya ligi ashirikishe ofisi yake na wachezaji wa lingi ya
mwaka 2018 wawe wenye umri 15 hadi 17 ili baada ya mashindano hayo baadhi ya
vijana watachukuliwa kujiunga na timu ya watoto ya taifa.
Mshindi
wa kwanza Runzewe Academy Fc ilikabiziwa kombe la ushindi wa Ligi ya Doto Cup
2017 yenye thamani ya sh 300,000 na kitita cha fedha Sh 500,000 seti tatu za
jenzi mipira mitatu cheti cha ushiriki.
Timu
ya Chui fc ya Bugelenga washindi wa pili walibeba sh 300,000 seti za jenzi
mbili mipilia miwili na cheti cha kushiriki huku mshindi wa tatu Kurugenzi fc
ya Katente walijinyakulia sh 200,000 seti ya jezi moja mpira moja na cheti cha ushiriki.
Comments
Post a Comment