ASKARI MWINGINE WA JWT ALIYESHAMBULIWA DRC AFARIKI DUNIA
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa
katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati
akipatiwa matibabu. Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania
waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi
wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani
wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa
Tanzania na watano wa DRC. Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa,
Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao
Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku. Katika taarifa
iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania
amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala. Umoja wa Mataifa
umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki
pamoja na serikali ya Tanzania kutokana na msiba huo.
Comments
Post a Comment