WAKAZI WA NG'ANZO-BUKOMBE WAUNGWA MKONO NA MHE. DOTO BAADA YA KUONYESHA JITIHADA ZAO KWA PAMOJA

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na Kamati ya Elimu Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe wakikagua Jengo la vyumba vya madarasa katika Shule ya msingi Mtakuja vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi.

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na Kamati ya Elimu Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe  kwenye mkutano wa hadhara  Kitongoji cha Mtakuja-Ng'anzo baada ya ukaguaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM(W)Bukome Nelvin Salabaga Ndugu akizungumza na Hadhara ya Mtakuja-Ng'anzo
  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mtakuja Ibrahim Paul Kinasa akiwa amesisima kungua mkutano. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Diwani wa Kata ya Iyogelo Mhe. Juma Lushiku akizungumza na wakazi wa Mtakuja.
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa Kitongoji cha Mtakuja-Ng'anzo baada ya kukagua baadhi ya maeneo yenye miradi ya maendeleo akiwa na  Kamati ya Elimu Afya na Maji Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
  Picha ya baadhi ya wananchi wakimsikiliza  Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb)



Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita,Mhe. Doto Mashaka Biteko
amewachagia gharama zote za saruji  ili kuhakikisha vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Kata ya  Ng’anzo  vinafikia hatua ya kupauliwa baada ya wananchi kutumia nguvu zao mpaka hatua ya renta na kumua kuwashika mkono.

Kabla ya Mbunge Doto kuchangia mradi wa maendeleo ulioibuliwa na wananchi
Biteko aliwashukuru kwa kumchangua siku ya uchaguzi Oktoba 25 mwaka
2015 na kwamba hawezi kumlipa mmoja mmoja kwa kazi yake na kusema atahakikisha
anawatumikia na kutetea wananchi wa Bukombe ili wapate maendeleo.

Wakati akiwapongeza wananchi wa Mtakuja kwa kuibua mradi wa kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo ya msingi uku akiwasihi kusomesha watoto wao ili kulinusuru taifa la kesho na kuwataka wananchi wanaojishughulisha na kilimo wasikubali kuuziwa na  wauzaji wa pembejeo kwa bei kubwa kwani serikali imetoa bei elekezi ili kuzuia mifumuko ya bei kwenye pembejeo hizo

Awali Diwani wa Kata ya Ng’anzo Mhe. Kipara Silantemi na baadhi ya wananchi wamezungumzia changamoto za Kitongoji cha Mtakuja na Kata nzima ya Ng’anzo ambazo ni ukosefu wa miundo mbinu ya barabara,baadhi ya wazee kushindwa kuwezeshwa fedha za TASAF,Wanafunzi wanao maliza Darasa la saba kutopewa vyeti vyao baada ya kuhitimu elimu hiyo na mifugo kukosa malisho baada ya idadi kubwa ya ya mifugo kutoka kwenye mapori ya hifadhi na kujaa vijijini.

Diwani wa Kata ya Iyogelo Mhe. Juma Lushiku ambaye ni mwenyekiti wa
Kamati ya Elimu Afya na Maji halmashauri ya Wilaya ya Bukombe aliwapongeza wananchi kwa hatua waliyoifikifikia katika ujenzi wa vyumba hivyo pamoja na kuwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao na kufika sehemu za huduma pale wanapo pata taarifa za ujio wa waalam ili kujua ya afya

Nae Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Mtakuja Ibrahim Paul Kinasa alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa kujitoa kwake na kwaomba wananchi kuzidi kujitoa na wao ili kumaliza changamoto zao za baadhi ya watoto kusomea nje.


Comments