KAMATI YA SIASA (CCM)-UYOVU WAKUTANA NA MHE. DOTO BITEKO

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na moja wa wajumbe wa Kamati ya Siasa (CCM) Kata ya Uyovu.
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Uyovu Ndg Mauba baada ya kuwasili Ofisini hapo ili kukitana na Wajumbe wa  Kamati ya Siasa wa Kata hiyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi  Kata ya Uyovu ndg Baraka Kayumbo akisema jambo.
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na Wajumbe Wa Kamati ya Siasa Kata ya Uyovu alisema "Hongereni sana kwa kuchaguliwa naomba tufafenye kazi kwa pamoja ili tujenge chama chetu kiwe imara kwa maslahi ya  taifa letu".
 Wajumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Uyovu wakiwa na wageni ambao ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (W)Bukombe Nelvin Salabaga Ndugu ,Afisa Elimu Shule za Msingi (W)Bukombe Shadrack Kabanga na Mratibu Elimu Kata ya Uyovu
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na Viongozi wa Uvccm Kata ya Uyovu pamoja na Vijana waliojitokeza kukutana na Mbunge wao baada ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi na kuwa Wanachama Wapya.

Comments