MBUNGE DOTO KUMALIZIA VYUMBA VYA MADARASA KANEMBWA-UYOVU

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na wadau wengine wa elimu wakijionea hali halisi ya darasa wanalosomea wanafunzi (Ni tukio la miezi 7 nyuma)
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akikagua jengo la darasa lililotelekezwa tangu 2013 lililokuwa likijengwa kwa nguvu za wananchi na kuchukua hatua ya kulimalizia kwa kutumia fedha zake binafsi (Ni tukio la miezi 7 nyuma).
   Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akielekea kuangalia jengo la darasa alilolifadhili  kwa kutumia fedha zake binafsi ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya kujifunzia baada ya kutembelea shule hiyo ya msingi Kanembwa  miezi saba nyuma na kukuta baadhi ya wanafunzi wakisomea kwenye jengo ambalo ni hatarishi na kuamua kulimalizia jengo jingine lililokuwa limeterekezwa tangu 2013 lililokuwa likijengwa kwa nguvu za wananchi.

 Muonekano wa Jengo hilo Hivi sasa baada ya Ufadhi wa Mhe. Doto Mashaka Biteko (Mb).

Comments