IGULWA KUNUFAIKA NA MRADI WA VISIMA KUTOKA PRF


Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni-Igulwa Yahaya Butalotwa(Mwenye Shati nyekundu) akiongozana na wafadhili wa mradi wa maji safi  Poverty Relief Fund(PRF) walipowasili kwa ajili ya uzinduzi wa Kisima
 Kisima kilichozinduliwa leo.


 Mmoja wa wakazi wa Mkuyuni akichota maji baada ya uzinduzi



 Wakazi wa Mkuyuni wakitumbuiza katika uzinduzi wa Kisima kilichofadhiliwa na PRF.
Mtendaji Mkuu wa Poverty Relief Fund(PRF) Fr. Honoratus Ndaula akizungumza na wakazi wa Mkuyuni, Kata ya Igulwa Wilayani Bukombe  amewasihi  wakazi hao kukitunza vizuri kisima hicho ili kiweze kudumu kwa mda mrefu na wapunguzia changamoto ya maji waliyokuwa nayo awali.

Ndaula ilisema huduma hiyo haina itikadi yeyote ya dini kwani kisima hicho ni kwa ajili ya jamii nzima hivyo kila mwanajamii ahusike kukilinda kisima hicho, sambamba na kubainisha maeneo yatakayo pata visima hivyo vya mradi kwa Kata ya Igulwa ambayo ni Mgombani,Mchangani,Kasaka B,Butambala,Buntubili, Imalamagigo na Rulembela na kwa upande wa Kata nyingine ni Lyambamgongo na Ng'anzo.
Diwani wa Kata ya Igulwa  Mhe.Richard Mabenga akizungumza na wakazi wa Mkuyuni kwenye Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Kisima.
 Mfadhili wa Mradi wa Maji Safi akikabidiwa Asali lita Tano na Wananchi wa Mkuyuni 
 Picha ya Viongozi watakaosimamia Kisima Cha Mkuyuni ili kuhakikisha kina kugumu kwa mda mrefu.
 Viongozi wa Poverty Relief Fund (PRF) na Diwani wa Kata ya Igulwa  Mhe.Richard Mabenga wakiwa Eneo la Mgombani Kata ya Igulwa kwa lengo la kutasimini namna ya kukiboresha kisima cha awali kuwa cha kisasa ili kiweze kutoa huduma ya maji safi kwa wakazi wa mgombani
  Viongozi wa Poverty Relief Fund (PRF) na Diwani wa Kata ya Igulwa  Mhe.Richard Mabenga wakiwa Eneo la Butambala  Kata ya Igulwa kwa lengo la kutasimini eneo ili waweze kuwafadhili mradi wa maji safi kwa maeneo hayo baada ya wakazi hao kuteseka kwa mda mrefu kwenye suala zima la maji safi








Comments