Serikali
ya Zimbabwe imemuombea mke wa Rais Mugabe kinga ya kidiplomasia dhidi ya
kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.
Taarifa
hizo zimetolewa na maofisa wa polisi wa taifa hilo leo asubuhi zikidai
hayo yamefanyika kwa mujibu wa sheria.Grace Mugabe alikuwa bado yupo
Afrika Kusiniā iliongezea wakipinga ripoti za awali kwamba alikuwa
amerudi nchini Zimbabwe.Taarifa ya mtandao wa BBC Swahili,imesema
kuwa,mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 amemtuhumu Grace Mugabe kwa
kumshambulia katika hoteli moja mjini Johannesburg.Polisi walitarajia
kwamba mke huyo wa Mugabe angejisalimisha kwao mwenyewe siku ya Jumanne
lakini hakufanya hivyo.Hata hivyo Afrika Kusini bado ilikuwa inataka
kuhakikisha kuwa kinga hiyo amepatiwa kulingana na sheria, ilisema
taarifa hiyo.Mazungumzo yalikuwa yanaendelea na mawawikili wa Mugabe na
ubalozi wa Zimbabwe kuhusu swala hilo, ilisema taarifa.Akizungumza mbele
ya kamati ya bunge mapema, Kaimu Mkuu wa Polisi Lesetja Mothiba alisema
kuwa Grace Mugabe anatakiwa aende mahakamni.
Hatahivyo,hajatoa tamko lolote tangu maaoisa wa polisi waanze kumchunguza kuhusu madai hayo ya unyanyasaji.
Comments
Post a Comment